Na: Hashim Jumbe
Ni kipindi cha mwaka mmoja sasa tangu Diwani wa Kata
ya Kipawa Mhe. Kenedy aingie madarakani, siku ya Jumamosi ya tarehe 10 Disemba,2016
Diwani Kenedy ameitumia siku hiyo kukutana na Wananchi wa Kata ya Kipawa kwa
lengo la kuwashukuru kwa kumchagua kuiongoza Kata hiyo kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka
2015 huku pia akitumia Mkutano huo kusikiliza kero na malalamiko mbalimbali yanayojitokeza kwenye Kata hiyo.
Katika Mkutano huo Mheshimiwa Diwani aliambatana na Muwakilishi
wa OCD-Ukonga, Mtendaji wa Kata ya Kipawa, Wenyeviti wa Mitaa mitatu ya Kipawa ambayo
ni Mtaa wa Karakata, Mji mpya na Mtaa wa Airport, halikadhila Mkutano huo pia
ulihudhuriwa na Wataalamu wa Mazingira kutoka Ofisi ya Mazingira Manispaa ya Ilala.
Waakati wa Mkutano huo,Wananchi walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali ikiwa ni pamoja na kueleza kero zinazowakabili kwenye Kata hiyo ambapo Mwenyekiti wa
Mkutano huo aliyatolea ufafanuzi na maswali mengine aliyaelekeza kwa Wataalamu alioambatana nao na kupatiwa majawabu ya papo kwa papo.
Maswali kama ya athari zipi zinazowezwa kuletwa kutokana na uharibifu wa bonde la mto Msimbazi eneo
la Karakata unaosababishwa na kuchimbwa kwa mchanga, tozo za uondoshwaji wa
takataka majumbani, kero za miundombinu na ushirikishwaji wa Wananchi kwenye
ulinzi na usalama yaliyoibua hisia za wengi kwenye Mkutano huo.
Aidha, kwenye Mkutano huo Afisa Mazingira kutoka
Ofisi ya Mazingira Manispaa ya Ilala, Mama Magesa alitumia nafasi hiyo kupiga
marufuku kufanyika kwa shughuli yoyote ya kimaendeleo kwenye sehemu ya hifadhi
ya bonde la Msimbazi ambapo kwa mujibu wa sheria za Uhifadhi wa Mazingira kwa
yoyote atakayepatikana akifanya shughuli za kimaendeleo kwenye eneo hilo
atakamatwa na kutozwa faini isiyopungua Elfu Hamsini na isiyozidi Milioni
Hamsini.
Diwani wa Kata ya Kipawa, Mheshimiwa Kenedy
akisikiliza moja ya maswali yaliyoulizwa kwenye Mkutano na Wananchi wa Kipawa
|
Baadhi ya Wananchi waliojitokeza kwenye Mkutano na
kutoa kero zao mbele ya Diwani Kenedy
|
Mtaalamu wa Mazingira kutoka Ofisi ya Mazingira
Manispaa ya Ilala, Mama Magesa akitoa ufafanuzi wa hoja ya uhifadhi wa
mazingira kwenye maeneo ya bonde la mto Msimbazi
|