MKURUGENZI MANISPAA YA ILALA ALIPOTEMBELEA SHULE ILIYOEZULIWA PAA

Na: Hashim Jumbe
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Ndugu Msongela Nitu Palela ametembelea shule ya Msingi Kigogo fresh na kujiona athari zilizoletwa na upepo mkali pamoja na mvua zilizonyesha siku ya jumatatu maeneo ya pembezoni mwa Kata za Manispaa ya Ilala.

Shule hiyo ya Msingi Kigogo fresh iliezuliwa paa kwenye jengo lenye madarasa matatu na ofisi moja ya Walimu, huku kadhia hiyo ikimuathiri Mwanafunzi mmoja aliyekuwa kwenye harakati za kujinusuru.

Aidha, Mkurugenzi Palela pia alipata fursa ya kumtembelea Mwanafunzi huyo aliyelazwa kituo cha afya cha Pugu Kajiungeni kwa matibabu ambapo alimkuta Mwanafunzi huyo akiendelea vizuri na kusubiri ruhusa ya Daktari.







Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi