Na:Anjelina P.Mapunda
Mstahiki Meya wa
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh.Charles Kuyeko akiambatana na
Viongozi wengine wa Serikali pamoja na Watendaji wa Halmashauri katika uzinduzi
wa daraja la Kinyerezi-Bonyokwa maeneo ya Kisiwani Jijini Dar es salaam.
Awali akizungumza katika
hafla hiyo Mhandisi wa Manispaa ya Ilala ndugu Benjamin Maziku alisema daraja hilo linauwezo
wakupitisha mzigo chini ya tani saba(7), lenye urefu wa mita 30 limejengwa
kwa takribani mwaka mmoja na kugharimu Tsh.million 478 hadi kukamilika kwake.
Ujenzi wa daraja hili umesua sua kwa siku nyingi kutokana na sababu mbali mbali
lakini kutokana na usimamizi imara wa Mstahiki Meya wa Ilala Mhe. Charles
Kuyeko sasa historia imebadilika
Mstahiki Meya alipata
fursa ya kuzindua daraja hilo linalounganisha Kata ya Bonyokwa na Kinyerezi, ambapo
kukosekana kwa kivuko hicho ilikuwa ni kero kwa Wananchi wa kata hizo mbili na
kuzuia mawasiliano pamoja na shughuli za maendeleo.
Katika uzinduzi huo Mstahiki
Meya alipata fursa ya kuzungumza na Wananchi na kuwasihi kuwa
Daraja hilo limejengwa na kodi zao,hivyo hawana budi kila Mwanachi awe mlinzi
wa mwenzie katika kulinda daraja hilo ili kufanikisha gurudumu la maendeleo
kusonga mbele katika kata hizo na Manispaa ya Ilala kwa ujumla.