Na: Anjelina P. Mapunda
Ubalozi
wa Kuwait nchini Tanzania ukishirikiana na Wadhamini kutoka Muslim Islamic Relief
Organization, wamekabidhi visima kumi
(10) vya maji kwaajili ya shule za Msingi Manispaa ya Ilala ikiwa ni utekelezaji
wa huduma ya maji kwa Wanafunzi
Awali
Kaimu Afisa Elimu Msingi Bw. Hamis Mlangala alisema “visima hivyo vyenye urefu zaidi ya mita 60 kwenda
chini vimechimbwa katika Kata tofauti zilizoko Manispaa ya Ilala, shule zilizonufaika na
visima hivyo ni pamoja na Bwawani, Yombo, Umoja, Mwale, Kitunda, Jitihana,
Serengeti, Mafuriko, Kombo na Vingunguti
Naye Balozi wa Kuwait nchini Tanzania alisema Visima
hivyo vitatatua changamoto zilizokuwa
zinawakabili Wanafunzi wa shule hizo. Pia aliongeza kwa kusema kuwa visima
hivyo inabidi vitunzwe na kuwa na matumizi mazuri ya maji kwa ajili ya manufaa ya vizazi vijavyo.