STANDARD CHARTERED WAPANDA MICHE YA MITI 400 SHULE YA MSINGI VIWEGE, WAKABIDHI NA KOMPYUTA 10

Na: Hashim Jumbe
Benki ya Standard Chartered mwaka huu wa 2017 ikiwa inatimiza miaka 100 tangu ianze kutoa huduma Nchini Tanzania, wameitumia siku ya leo kupanda miche ya miti 400 yenye matunda na miti yenye kuleta vivuli Shule ya Msingi Viwege pamoja na kukabidhi Kompyuta 10 zitakazotumika kufundishia somo la TEHAMA shuleni hapo.

Standard Chartered ni miongoni mwa Wadau wakubwa wa elimu na uhifadhi wa mazingira kwa Manispaa ya Ilala, ikiwa sasa ni mwaka wa nne tangu waanzishe kampeni ya kupanda miche ya miti kwa Shule za Msingi za Manispaa ya Ilala.

Kampeni ya upandaji miti 20,000 pamoja na kutoa kompyuta kwa Shule za Msingi Manispaa ya Ilala, tangu ianze hadi sasa Standard Chartered wameshapanda miche ya miti 400 kwa Shule ya Msingi Pugu Kajiungeni, miche ya miti 350 pamoja na kompyuta 10 kwa Shule ya Msingi Kimwani, miche ya miti 350 na kompyuta 10 kwa Shule ya Msingi Buyuni.

Shule nyengine zilizonufaika na msaada huo ni pamoja na Shule ya Uhuru Mchanganyiko na Shule ya Msingi Kigogo fresh ambazo nazo kila moja zilipata kompyuta 10 na miche ya miti 350




Afisa Elimu Manispaa ya Ilala Bi. Elizabeth Thomas ambaye amemuwakilisha Mgeni Rasmi  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema akitoa salamu za Mkuu wa Wilaya wakati wa zoezi la kupanda miche ya miti shule ya Msingi Viwege


Muwakilishi wa Benki ya Standard Chartered ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti cha Benki ya Standard Chartered Bw. Abdulsamad Abdul akitoa salamu kwa niaba ya benki hiyo


Muwakilishi wa Benki ya Standard Chartered ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti cha Benki ya Standard Chartered Bw. Abdulsamad Abdul aliyesimama upande wa kulia, akimkabidhi kompyuta Mkuu wa Shule ya Msingi Viwege, Mwalimu Ferdnand  Nyambaya

Muwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala ambaye ni Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala Bi. Elizabeth Thomas akipanda mti shule ya Msingi Viwege
Muwakilishi wa Benki ya Standard Chartered ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti cha Benki ya Standard Chartered Bw. Abdulsamad Abdul akishiriki kwenye upandaji wa mti shuleni Viwege




Wanafunzi wa Shule ya Msingi Viwege wakipanda miche ya miti shuleni kwao

1 Maoni

  1. Hongera Viwege mtumie kuongeza tija hapo shuleni fursa mmepata tumia

    JibuFuta
Mpya zaidi Nzee zaidi