WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ALIVYOKABIDHI VIFAA VYA KUJIFUNZA NA KUJIFUNZIA KWA SHULE ZENYE MAHITAJI MAALUM

Habari picha na Hashim Jumbe
Mkuu wa Mkoa wa DSM Mhe. Paul Makonda wa kwanza kulia, akisalimiana na Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Mhe. Omary Kumbilamoto alipowasili Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko kushuhudia makabidhiano ya vifaa vya kujifunzia na kufundishia kwa shule zenye mahitaji maalum, pembeni yao ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema
Mkuu wa Mkoa wa DSM, Mhe. Paul Makonda wa pili kushoto akifurahia jambo sambamba na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la DSM wa kwanza kulia Bi. Sipora Liana, akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Ally Hapi, Mkurugenzi OR-TAMISEMI Bi.Mushi na wa kwanza kushoto ni Naibu Meya Manispaa ya Ilala Mhe Omary Kumbilamoto
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Tawala Mkoa wa DSM, Bi. Theresia Mmbando, alipowasili kwenye makabidhiano ya vifaa vya kujifunzia na kufundishia kwa shule zenye uhitaji maalum
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako aliyesimama upande wa kulia, akioneshwa zana zinazotumika kujifunzia kwa shule zenye uhitaji maalum Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko na Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala, Bi. Elizabeth Thomas, anayeshuhudia ni Afisa Elimu Mkoa wa DSM

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Bw. Msongola Palela wa kwanza kulia akiwa na Katibu Tawala Wilaya Ilala Bw.Edward Mpogolo wakifuatilia kwa karibu tukio la kukabidhiwa vifaa vya kujifunzia na kufundishia kwa Shule zenye uhitaji maalum

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akifanya utambulisho kwa Mgeni Rasmi Mhe. Kassim Majaliwa
Naibu Meya Manispaa ya Ilala pamoja na Wakuu wa Wilaya kutoka Temeke, Kigamboni na Kinondoni wakifuatilia tukio la kukabidhi kwa vifaa vya kujifunzia na kufundishia kwa shule zenye uhitaji maalum
Wanafunzi wa shule yenye uhitaji maalum ya Uhuru Mchanganyiko wakitoa burudani wakati wa shughuli za kukabidhiwa kwa vifaa kwa shule hizo






Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa DSM amabye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema akitoa salamu za Mkoa kwa Mgeni Rasmi Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa shughuli ya kukabidhi kwa vifaa shule zenye uhitaji maalum
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknojia, Profesa Joyce Ndalichako akitoa neno la ukaribisho kwa Mgeni Rasmi Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akihutubia wakati wa shughuli ya kukabidhi vifaa vya kujifunzia na kufundishia kwa shule zenye uhitaji maalum




Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akikata utepe kuashiria kukabidhi kwa vifaa vya kujifunzia na kufundishia kwa shule zenye uhitaji maalum

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimkabidhi vifaa hivyo Afisa Elimu Mkoa wa DSM
Waziri Mkuu Mhe.Majaliwa akikabidhi vifaa kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala





Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi