KATIBU TAWALA MKOA WA DODOMA AFUNGA MAFUNZO YA UTAWALA BORA KWA MADIWANI TOKA MANISPAA YA ILALA

Na: Hashim Jumbe-Dodoma
Katibu Tawala Mkoa wa Dododma, Bi. Rehema Madenge ameyafunga rasmi mafunzo ya siku tano juu ya Utawala Bora, waliyokuwa wakiyapata Madiwani kutoka Manispaa ya Ilala kwenye Chuo cha Serikali za Mitaa kilichopo Hombolo-Dodoma.

Wakati wa mafunzo hayo, Madiwani wa Manispaa ya Ilala walijifunza mada zifuatazo; Historia ya Serikali za Mitaa, Uongozi na Utawala Bora, Mpango wa Taifa wa Fedha za Miradi ya Maendeleo (LGDG), Mpango wa Fursa na Vikwazo (O&OD) Ulioboreshwa, Sheria za Serikali za Mitaa, Manunuzi na Usimamizi wa Mikataba katika MSM, Mahusiano ya TAMISEMI na MSM.

Mada nyengine walizojifunza ni pamoja na; Uwajibikaji wa Kijamii, Taratibu za Uendeshaji wa Vikao na Mikutano, Usimamizi wa Rasilimali Watu katika MSM, Sheria ya Ardhi, Usimamizi na Udhibiti wa Fedha, Kanuni za Maadili ya Madiwani, Majukumu, Wajibu, Haki na Stahiki za Madiwani, Changamoto za Uendeshaji wa MSM, Umuhimu wa kutambua Jitihada za Jamii na Umuhimu wa Maandalizi ya Jamii, Ngazi mbalimbali za Jitihada za Jamii kwa uendelevu wa Miradi ya Jamii.


Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Tafiti na Ushauri kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa, Dr. Michael Msendekwa akitoa taarifa fupi ya mafunzo mbele ya Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Bi. Rehema Madenge
Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa, Dr. Mpamila Madale akizungumza maneno mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kuzungumza na Madiwani kutoka Manispaa ya Ilala waliomaliza mafunzo ya Utawala Bora Chuoni hapo
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Bi. Rehema Madenge akizungumza na Wahitimu wa Mafunzo ya Utawala Bora ambao ni Madiwani kutoka Manispaa ya Ilala





Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya Utawala Bora, Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala, Mhe. Charles Kuyeko























 

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi