MABINGWA WA UMITASHUMTA MKOA WA DSM WAPOKELEWA KISHUJAA NA BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA ILALA

Na: Hashim Jumbe
Mabingwa wa UMITASHUMTA Mkoa wa DSM kwa mwaka 2017 timu ya Wilaya ya Ilala, wamepokelewa kishujaa na Baraza la Madiwani Manispaa ya Ilala baada ya kuchukua ubingwa wa UMITASHUMTA Mkoa wa DSM kwa mwaka 2017.

Katika mashindano hayo yaliyofanyika mapema mwezi Julai mwaka huu, Wilaya ya Ilala walishinda kikombe cha mpira wa miguu kwa Wavulana, ubingwa wa mpira wa miguu maalum kwa Wavulana, ubingwa wa mpira kwa Vipofu upande wa Wavulana na upande wa Wasichana 'goalball', ubingwa wa jumla wa riadha, na ubingwa wa jumla wa mashindano kwa mwaka 2017.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala ambaye ni Afisa Elimu Msingi, Bi. Elizabeth Thomas akiitambulisha timu ya UMITASHUMTA ya Wilaya ya Ilala kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Ilala
Kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Ilala kikisikiliza utambulisho wa Ugeni wa Mabingwa wa  UMITASHUMTA kwa Mkoa wa DSM kwa mwaka 2017
Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala akipokea kombe la ubingwa wa mpira wa miguu kwa Wanafunzi maalumu
Mstahiki Meya akipokea kombe la ubingwa wa mpira wa miguu
Mstahiki Meya wa Ilala, Mhe. Charles Kuyeko akipokea kombe la ubingwa wa mchezo wa vipofu 'goal ball'



Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala, Mhe. Charles Kuyeko akipokea kombe la ushindi wa jumla kwa mashindano ya UMITASHUMTA Mkoa wa DSM yaliyofanyika mapema mwezi Julai. Kombe hilo lilichukuliwa na timu ya Wilaya ya Ilala
Vikombe vilivyokabidhiwa kwa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Ilala kama vinavyoonekana

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi