MADIWANI MANISPAA YA ILALA WAHUDHURIA MAFUNZO YA UONGOZI CHUO CHA SERIKALI ZA MITAA-HOMBOLO

Na: Hashim Jumbe-Dodoma
Madiwani kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, leo wameanza mafunzo ya siku tano yanayofanyika Chuo cha Serikali za Mitaa-Hombolo, huku mafunzo hayo yakilenga kuwajengea uwezo kwenye maeneo ya Uongozi na Utawala Bora, Usimamizi wa fedha za Umma, Manunuzi na Usimamizi wa Mikataba katika ngazi za chini, Sheria za Serikali za Mitaa, Uwajibikaji  wa Kijamii, Taratibu za uendeshaji wa vikao na mikutano, Kanuni za Maadili ya Madiwani.

Maeneo mengine wanayotarajia kujifunza ni pamoja na, Majukumu, wajibu, haki na stahiki za Madiwani, Mpango wa fursa na vikwazo (O & OD) iliyoboreshwa na Usimamizi wa Rasilimali Watu katika MSM
Madiwani kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala walioshiriki kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo kwenye masuala ya Uongozi yanayofanyika kwenye chuo cha Serikali za Mitaa-Hombolo
Mstahiki Meya kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mhe. Charles Kuyeko akitambulisha Ugeni alioambata nao kwenye mafunzo hayo.













Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi