MADIWANI MANISPAA YA ILALA WATEMBELEA MASHAMBA YA ZABIBU YALIYOPO HOMBOLO NA KISHA WAPATA ELIMU YA ULIMAJI

Na: Hashim Jumbe-Dodoma
Ni wastani wa mwendo wa Kilomita 42 kutokea katikati ya Mji wa Dodoma, ndipo kilipo Chuo cha Serikali za Mitaa maarufu kama Hombolo. Chuo hiki kinachosifika kwa elimu ya uendeshaji na usimamizi wa Serikali za Mitaa, safari hii kimepata nafasi ya kutembelewa na Madiwani kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala waliofika kwa lengo la kupata mafunzo ya usimamiaji bora wa Halmashauri.

Pamoja na mafunzo wanayoendelea kuyapata chuoni hapo, lakini pia Waheshimiwa Madiwani wamepata nafasi ya kutembelea mashamba yanayolimwa zabibu yaliyopo jirani na chuoni hapo, na kujifunza namna bora wanayoweza kuitumia kwa ajili ya kilimo cha zabibu.

Wakiwa kwenye mashamba ya zabibu, walijifunza namna zao hilo linavyoanza kuandaliwa, njia ya kuhifadhi zao hilo lisishambuliwe na wadudu na mpaka hatua ya uvunaji inavyofika.

Aidha, ziara hiyo pia iliwapa nafasi Waheshimiwa Madiwani kutembelea kiwanda kinachotengeneza mvinyo unaotokana na zabibu zinazolimwa kwenye mashamba yaliyopo Hombolo
















Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi