MANISPAA YA ILALA YAPATA HATI SAFI

Na Neema Njau
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imepata hati safi ya ukaguzi wa hesabu za Serikali kwa kipindi cha mwaka 2015/2016. Hayo yamesemwa na Bwana Patrick Malando Lugisi ambaye ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika kanda ya Ilala wakati akiwasilisha taarifa ya ukaguzi wa mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2015/2016 katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani cha Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kilichofanyika tarehe 24 Agosti, 2017 katika ukumbi wa Mikutano wa Arnatoglou.


Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mheshimiwa Charles Kuyeko akifungua Kikao cha Baraza la Madiwani

Mkuu wa Idara ya Fedha na Biashara Bwana Tulusibya Kamalano akimwakilisha Mkurugenzi katika Kikao cha Baraza la Madiwani

Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Bibi Theresia Mmbando akiongea akiongea kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa katika kikao hicho

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika kanda ya Ilala Bwana Patrick Malando Lugisi akiwasilisha Taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali katika kikao cha Baraza la Madiwani

Baadhi ya Wajumbe wa Kikao cha Baraza la Madiwani 

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi