WATUMISHI MANISPAA YA ILALA WATUMIA MAPUMZIKO YA MWISHO WA JUMA KUTEMBELEA MBUGA YA MIKUMI

Na: Hashim Jumbe-Mikumi
Ni umbali wa takribani Kilomita 295 kutokea upande wa Magharibi mwa Mji wa DSM ndipo uweze kufika kwenye Mbuga ya Mikumi, ambayo ni hifadhi ya Nne kwa ukubwa wa eneo Nchini Tanzania, hivyo itakupasa utumie masaa yasiyopungua Matano hadi Sita kwa mwendo wa wastani kama unatumia usafiri wa njia ya barabara kutokea DSM.

Mbuga ya Mikumi ambayo ilianzishwa mwaka 1964 iliitwa jina hilo kutokea katika jina la asili la eneo ilipo Mbuga hiyo, ambalo ni 'Mikumi' huku Mbuga hiyo ikiwa na vivutio mbalimbali vya Wanyamapori kama vile; Tembo, Twiga, Simba, Swala, Nyati na Wanyama wengineo mbalimbali, huku Mbuga hiyo ikikadiriwa kuwa na ukubwa wa Kilomita za Mraba 3,230.

Lakini pamoja na Tanzania kuwa Nchi yenye baraka kwa kuwa na vivutio vingi vya kiutalii kama vile hifadhi za Mbuga za Wanyama, lakini miongoni mwa mambo yanayoirudisha nyuma sekta hii ni pamoja na muitikio hafifu wa Watanzania wanaotembelea maeneo hayo, ingawaje Serikali imekuwa ikitenga bajeti kubwa kutangaza maeneo yenye vivutio.

Kwa kutambua umuhimu wa kutembelea maeneo yenye vivutio Nchini mwetu na kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano ya kukuza pia sekta hii ya Utalii, ndipo Watumishi kutoka Manispaa ya Ilala waliposukumwa na nia ya kutembelea maeneo hayo yenye vivutio huku wakiwa na lengo la kujifunza na kujionea ufahari wa Nchi yao ya Tanzania.

Katika ziara hiyo, Watumishi kutoka Manispaa ya Ilala walitembelea maeneo mbalimbali wakiwa kwenye hifadhi ya Mbuga ya Mikumi, huku wakipata pia fursa ya kuuliza maswali mbalimbali yaliyowajengea uwezo wa kufahamu maisha ya viumbe mbalimbali vinavyoishi kwenye Mbuga hiyo, hivyo ziara hiyo imewazidishia pia ari ya kujivunia Nchi yao na Rasilimali zilizopo






















Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi