Na:Hashim Jumbe
Kamati ya Fedha na Utawala ya Manispaa ya Ilala, imefanya ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo iliyotekelezwa kwa kipindi cha robo ya kwanza ya kuanzia Julai hadi Septemba, 2017. Kamati hiyo iliyo na jukumu la kuhakikisha Miradi yote ya Maendeleo inayotekelezwa kwenye Halmashauri inapata usimamizi wa kutosha ikiwa pamoja na kupima thamani halisi ya fedha zinazotumika kwenye Miradi hiyo.
Wakati wa ziara hiyo, Kamati ya Fedha na Utawala ilipata nafasi ya kukagua Miradi mbalimbali ikiwemo ya Maji na Barabara. Miradi yote iliyotembelewa ni kama ifuatayo;

- Ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa Mvuleni iliyopo Kata ya Msongola; Ujenzi wa Ofisi hii utanufaisha Wananchi wapatao 2,141 ambao watapata huduma katika Ofisi hii, gharama za Mradi ni Shilingi Milioni 45.
- Ujenzi wa barabara ya Segerea-Bonyokwa iliyopo Kata ya Bonyokwa: Kukamilika kwa ujenzi wa barabara hii utawarahisishia usafiri Wananchi waendao Bonyokwa, Segerea, Kinyerezi na Kimara. Gharama za Mradi ni Shilingi Bilioni 1.9
- Ujenzi wa Kisima na Miundombinu ya Maji; Ujenzi wa Mradi huu unatarajiwa kuwahudumia Wananchi wapatao 1,500 kutoka Kata ya Segerea. Gharama za Mradi ni Shilingi Milioni 53.5
- Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya DMDP; Ujenzi huu wa jengo la ghorofa 3 kwa ajili ya Ofisi za DMDP. Gharama za Mradi ni Shilingi Bilioni 1.1 na Mradi huu utawanufaisha Watumishi kuwa na Ofisi nadhifu na mazingira yaliyoboreshwa kwenye kufanyia kazi.