Na: Hashim Jumbe
Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii ya Manispaa ya Ilala, chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Jacob Kissi imefanya ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo iliyotekelezwa kwa kipindi cha robo ya kwanza ya Julai-Septemba, 2017, ambapo ziara hiyo ilijikita kuangazia Miradi iliyotekelezwa kwenye Sekta ya Elimu pamoja na Sekta ya Kilimo.
Wakati wa ukaguzi wa Miradi hiyo, Kamati ilipata nafasi ya kuangalia Miradi iliyotekelezwa pamoja na kupima thamani ya Miradi hiyo, na kisha kushauri kwenye Miradi imbayo utekelezaji wake unaendelea.
Miradi iliyotembelewa na Kamati hiyo ni kama ifuatayo;

- Ujenzi wa choo cha ghorofa Shule ya Msingi Bunge, Mradi huu kukamilika kwake utawasaidia Wanafunzi 2,155 kuweza kupata huduma ya choo. Gharama za Mradi huu ni Shilingi Milioni 62.9 na unatekelezwa kwa fedha za Halmashauri.
- Ukarabati wa vyumba 6 vya Madarasa Shule ya Sekondari Kasulu, Mradi huu utasaidia Wanafunzi 240 kupata madarasa ya kusomea. Gharama za ukarabati ni Shilingi Milioni 104 na unatekelezwa kwa fedha za Halmashauri.
- Ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na vyoo Shule ya Msingi Karakata, Mradi huu utasaidia kupunguza msongamano wa Wanafunzi katika vyumba vya madarasa. Gharama za Mradi ni Shilingi Milioni 66.6 na Mradi unatekelezwa kwa fedha za ufadhili toka Benki ya Dunia.
- Uendelezaji wa Kituo cha usindikaji mazao Kinyamwezi, Mradi huo utasaidia kufundishia shughuli za usindikaji wa mazao. Gharama za Mradi ni Shilingi Milioni 309.8 na Mradi unatekelezwa kwa fedha za Halmashauri.
- Ujenzi wa Madarasa manne Shule ya Msingi Kidugalo, Mradi huu utasaidia kupunguza msongamano na umbali wa Wanafunzi kufuata shule. Gharama za Mradi ni Shilingi Milioni 110 na Mradi unatekelezwa kwa fedha za Halmashauri.
Wajumbe wa Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii pamoja na Watendaji wa Manispaa ya Ilala wakipitia taarifa wakati wa ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo |
Choo cha ghorofa kinachoendelea kujengwa Shule ya Msingi Bunge |
Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji Manispaa ya Ilala, Bw. Ando Mwankunga akiwa mbele kuingia kwenye moja kati ya madarasa 6 yaliyofanyiwa ukarabati Shule ya Sekondari Kasulu |
Madarasa 6 yaliyofanyiwa ukarabati Shule ya Sekondari Kasulu |
Madarasa matatu Shule ya Msingi Karakata yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia |
Ujenzi wa kituo cha usindikaji mazao Kinyamwezi ukiwa kwenye hatua za awali |
Madarasa manne yanayojengwa Shule ya Msingi Kidugalo iliyopo Kata ya Chanika yakiwa kwenye hatua za mwisho |