WAZIRI JAFFO ARIDHISHWA NA MAANDALIZI YA UJENZI BARABARA YA MNYAMANI

Na: Tabu Shaibu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo amekagua  maandalizi ya  ujenzi  wa  Barabara ya Mnyamani  hadi Vingunguti na  kusema kuwa ameridhika na maandalizi ya ujenzi wa barabara hiyo.  Mhe Jaffo alifanya ukaguzi huo tarehe 23/01/2018 ikiwa ni takribani majuma mawili yamepita tangu alipoitembelea barabara hiyo na kujionea ubovu uliokuwepo. Katika Maagizo yake aliyoyatoa aliitaka Manispaa ya Ilala, Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini na DAWASCO kushirikiana pamoja na kuhakikisha kuwa Barabara hiyo inajengwa upya ili kuondokana na kero iliyokuwa ikisababishwa na ubovu wa barabara hiyo.  

Aidha Mhe Jaffo  ameelekeza kuwa Mkandarasi atakeyetekeleza kazi hiyo ahakikishe anatekeleza katika muda unaotakiwa kwa viwango bora. Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema  ambaye aliongozana na Mhe Jaffo katika ukaguzi wa maandalizi hayo amewakikishia wananchi wa maeneo ya Buguruni na Vingunguti kuwa Serikali itaendelea kusimamia ahadi zake ili kila mwananchi aweze kuishi maisha bora yenye kuinua uchumi wao. 


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi