WAGENI KUTOKA NCHINI CANADA WAITEMBELEA SHULE YA MSINGI UHURU MCHANGANYIKO

Na Neema Njau

Timu ya ushawishi ya kuchangisha wadau wa elimu "Global Education Partnership"inayotambulika kama One Campaign ya nchini Canada imeitembelea shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.

Ugeni huu uliopokekewa na kuhudhurishwa katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko na Mratibu Msaidizi wa  Programu ya LANES kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imekuja kwa ajili ya kukagua na kuona michango mbalimbali iliyotolewa na wafadhili mbalimbali kutoka Canada inavyoisaidia katika sekta ya elimu kupitia "Global Education Partnership".

Aidha ufadhili unaotolewa na wadau hao kutoka nchini Canada ni pamoja na Vitabu ambapo katika shule ya hiyo vilipokelewa Vitabu 321,miongozo 33 na mitaala 13 kwa darasa la kwanza hadi la tatu, Mafunzo kwa walimu 13 waliopatiwa mafunzo ya KKK  mafunzo ya kuboresha na kuondoa kabisa wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika pamoja na mafunzo kwa kamati ya shule yaliyolenga  kamati kufanya kazi ili kuleta  maendeleo ya shule.



Mwakilishi wa Afisa Elimu Msingi Bibi Asha Mapunda akiipokea Timu ya Ushawishi toka Nchini Canada walipowasili katika shule ya Msingi  Uhuru Mchanganyiko


Afisa  Elimu ya watu wazima Mkoa wa Dar es Salaam Bibi Benadetha Thomas akitoa neno la ukaribisho kwa Timu ya Ushawishi kutoka nchini Canada

Mratibu Msaidizi programu ya LANES kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia akitoa ufafanuzi juu ya utaratibu wa utoaji vitabu mbalimbali mashuleni.
Wajumbe wa Timu ya Ushawishi  kutoka nchini Canada wakifuatilia kwa umakini Uwasilishaji wa Taarifa mbalimbali.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko Bibi Anna Mshana (wa kwanza kulia) akiongoza wajumbe wa Timu ya Ushawishi kutoka nchini Canada  Kukagua maeneo mbalimbali ya shule hiyo.
Wanafunzi wa  Darasa la nne katika shule hiyo  waliotembelewa na Timu ya Ushawishi kutoka nchini Canada
Picha ya pamoja ikiwa Timu ya Ushawishi, Kamati ya Shule pamoja na wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi