Na: Hashim Jumbe
Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Selemani Said Jafo leo amefanya ziara ya ukaguzi na kuangalia athari zilizosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam na kisha Waziri huyo akatoa maagizo na maelekezo kwa Wananchi na Viongozi wa Halmashauri na Mkoa.
Wakati wa ziara hiyo Mhe. Jafo alitembelea eneo la Jangwani na kuangalia eneo hilo lilivyokumbwa na kadhia ya mafuriko kiasi cha kusababisha usumbufu na uharibifu wa Miundombinu iliyopo maeneo hayo, eneo jengine alilotembelea leo hii ni eneo la Ulongoni 'A' na 'B' Kata ya Gongolamboto.
Maagizo yaliyotolewa na Mhe. Selemani Jafo siku ya leo ni haya yafuatayo;

- Wananchi tuwe tunasikiliza Serikali inapotoa maelekezo, maelekezo haya haswa kupitia wenzetu wa Idara ya Hali ya Hewa walizungumza tokea mwanzo walioko katika maeneo ya mabondeni waweze kuondoka, mvua hizi zinaendelea kunyesha na si hapa tu Dar es Salaam athari hizi tumeziona Morogoro, Arusha, Katavi kila eneo.
- Ni marufuku Mtu yoyote kufanya shughuli za mchanga na DC ukikuta Watu kama hao kamata na weka ndani kwa sababu leo hii Serikali tunapata gharama ya kutengeneza Madaraja haya tena, kumbe ni kwa ajili ya Watu wachache ambao hata nyie Wananchi mnaona. Fikiria upande wa pili kama kuna Mama Mjamzito anatakiwa aende Hospitali anaendaje?
- Gharama tunayokuja kutumia hapa tutatumia kubwa sana, kwa hiyo nitoe maelekezo ni marufuku kwa Watu wote kuchimba mchanga katika Mto Msimbazi na pembezoni mwa mto. Hatuwezi kukubali Serikali kutumia gharama kubwa sana kwa uzembe wa Watu wachache.
- Serikali itafanya kila liwezekanalo Wananchi waweze kupita eneo hili, lakini ajenda yangu ipo palepale Wananchi waache kwa makusudi kuharibu mazingira.
- Nimeshaongea na mwenzangu Waziri wa Ulinzi na siyo muda mrefu Jeshi la Ulinzi litakuja huku kufanya tathmini eidha kati ya leo au kesho watakuja kufanya tathmini ya kutuwekea madaraja haraka kwa ajili ya Wananchi waweze kupita.