KAMATI YA UCHUMI NA HUDUMA ZA JAMII MANISPAA YA ILALA YATEMBELEA MIRADI ILIYOTEKELEZWA KWA KIPINDI CHA JANUARI-MACHI, 2018

Na: Hashim Jumbe
Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii Manispaa ya Ilala, leo imetembelea Miradi ya Maendeleo iliyotekelezwa na Manispaa hiyo kwa kipindi cha robo ya tatu ya kuanzia Januari hadi Machi kwa mwaka huu wa fedha 2017/2018.

Kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Jocob Kissi ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongolamboto, imefanya ziara kwenye Miradi ya Sekta ya Elimu, ambapo iliweza kutembelea Miradi minne inayosimamiwa na Idara ya Elimu Msingi na Mradi mmoja unaosimamiwa na Idara ya Elimu Sekondari.

Mradi uliotembelewa kwa Idara ya Elimu Sekondari ni Mradi wa Ujenzi wa Madarasa ya ghorofa Shule ya Sekondari Gerezani yanayotarajiwa kukakamilika ifikapo mwezi Juni, 2018 huku gharama za Mradi huo zikiwa ni Shilingi Milioni 300 kutoka kwenye makusanyo ya ndani ya Halmashauri.

Aidha, kwa upande wa Elimu Msingi, miradi iliyotembelewa ni pamoja na ukarabati wa majengo ya zamani katika Shule ya Msingi Mchikichini, Uhuru Mchanganyiko, Ilala na Msimbazi









Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi