Na: Hashim Jumbe
Ni miaka Sita (6) sasa tangu Manispaa ya Ilala kupitia Idara ya Elimu Msingi walipoanzisha mahusiano na Benki ya Kibiashara ya Standard Chartered, inayotoa huduma nchini Tanzania tangu kuanzishwa kwake mwaka 1917.
Katika kipindi hicho, Benki ya Standard Chartered imekuwa ikishirikiana na Idara ya Elimu Msingi Manispaa ya Ilala kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa shule za msingi zilizopo Manispaa ya Ilala kupitia kampeni yake ya upandaji miti 20,000 kwa mwaka nchi nzima.
Aidha, tangu kuanza kwa kampeni hiyo, shule kadhaa za Manispaa ya Ilala zimenufaika na upandaji wa miche ya miti ya matunda na miti kwa ajili ya vivuli, shule zilizonufaika hadi sasa ni Shule ya Msingi Pugu Kajiungeni ambapo ilipandwa miche ya miti 400, shule nyengine ni pamoja na Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Kigogo Freshi, Buyuni, Kimwani na Majani ya Chai, kila shule ilipandwa miche ya miti 350.
Shule nyengine iliyonufaika na kampeni hiyo hadi sasa ni Shule ya Msingi Yongwe, ambapo ilipandwa miche ya miti 400 pamoja na kupewa Viti 10 na Meza 10 ikiwa ni sehemu ya Benki hiyo katika kushiriki kwenye masuala ya Kijamii (Corparate Social Responsibility)
Halkadhalika, Shule za Msingi za Kimwani, Kigogo Freshi, Viwege na Buyuni zote zimenufaika na msaada wa Komputa 10 kila shule kutoka kwa Benki hiyo ya Standard Chartered, na leo Benki hiyo ilitoa tena Komputa 15, meza 8 pamoja na kupanda
miche ya miti 600 kwa shule ya msingi Yange Yange ikiwa ni muendelezo wa mahusiano na Manispaa ya Ilala