Na: Hashim Jumbe
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema leo amefungua rasmi mashindano ya umoja wa michezo na taaluma kwa shule za msingi Tanzania, maarufu kama UMITASHUMTA kwa ngazi ya Wilaya ya Ilala.
Mashindano hayo yanayofanyika kwa siku 3 kwenye viwanja vya Magereza vilivyopo Ukonga, yalianza mapema mwezi wa Aprili kwa kushindanisha madarasa, shule, kata na hatimaye kufikia kutengeneza timu za Klasta.
Aidha, kwa ngazi ya Wilaya, mashindano hayo yanashindanisha timu kutoka katika Klasta 4, ambazo ni Chanika, Ukonga, Kimanga na Gerezani, huku yakihusisha mchezo wa mpira wa miguu kawaida kwa Wavulana na Wasichana, mpira wa miguu kwa Wanafunzi wenye ulemavu-viziwi, riadha Wavulana na Wasichana, mpira wa pete, mpira wa mikono Wavulana na Wasichana, mpira wa wavu Wavulana na Wasichana.
Wakati huo huo, mashindano hayo yanatoa fursa ya kutengeneza timu itakayoiwakilisha Wilaya ya Ilala katika mashindano kwa ngazi ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Lakini, ikumbukwe kuwa timu ya Wilaya ya Ilala ndiyo inayoshikilia ubingwa wa UMITASHUMTA kwa ngazi ya Mkoa wa DSM kwa miaka mitatu (3) mfululizo, hivyo kuwa na nafasi nzuri kwa mwaka huu kushinda kwa mara ya nne (4) mfululizo.