Na: Hashim Jumbe
Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania, maarufu kama UMITASHUMTA kwa ngazi ya Wilaya ya Ilala yamehitimishwa jioni ya leo kwa timu ya Wilaya ya Ilala kuundwa.
Mashindano hayo kwa mwaka huu wa 2019 yameshirikisha timu Nne (4) kutoka katika Klasta za masomo za Chanika, Gerezani, Ukonga na Kimanga, yamefikia tamati kwa kutoa fursa kwa Wachezaji 130 kuingia katika timu ya Wilaya ya Ilala
Aidha, wachezaji hao ni wa mpira wa miguu wavulana (18) wasichana (16), mpira wa miguu kwa wanafunzi wenye ulemavu-viziwi (14), mpira wa mikono wavulana (10) wasichana (10), mpira wa wavu wavulana (9) wasichana (9), mpira wa pete (12), riadha (12) na fani za ndani wanafunzi 20
Hivyo, jumla ya wachezaji 130 wameianza kambi ya siku 10 kujiandaa na mashindano hayo kwa ngazi ya Mkoa wa Dar es Salaam yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mapema mwezi ujao.