Na, Judith Damas
Mkuu wa Wilaya
Mh. Ludigija ameyasema hayo leo tarehe
25 Januari 2021 alipokutana na wananchi
wa Kata ya Kipawa mtaa wa Stakishari katika ziara yake ya kutembelea bonde hilo
la Msimbazi ambalo limeleta changamoto kwa wananchi wa mtaa huo wakilalamika
kuhusu zoezi hilo la kutengteneza bonde hilo linavyofanyika .
Aidha wananchi
wa eneo hilo wakitoa malalamiko yao kwa
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.Ng’wilabuzu Ludigija juu ya zoezi hilo
linavyowaletea madhara makubwa ikiwemo mafuriko, kuharibika kwa miundombinu
kama barabara zao na kusababisha
uharibifu wa miundombinu ya umeme kwani magari yanayopita katika eneo hilo ni
makubwa na yanabeba mzigo mkubwa.
Akipokea hoja
hizo za wananchi Mkuu wa Wilaya ya Ilala amewaomba wananchi hao wawe wavumilivu
hadi taasisi hizo zitakapo kutana na kujadiliana kuhusu zoezi hilo.
“Naagiza taasisi
zote za Serikali ikiwemo TARURA,NEMC,TANROAD,Bonde la mto wami na idara
ya mazingira Manispaa ya Ilala zikutane na zijadiliane kama zoezi hili linalofanyika
lina tija katika kuzuia mmomonyoko na mafuriko, na ifikapo Ijuumaa January 29/2021 nipate
mrejesho kama zoezi hilo liendelee au lisitishwe ili kuzuia athari
zitakazotokea”.amesema hayo mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Ludigija
Aidha Mkuu wa
wilaya ya Ilala Mh.Ng’wilabuzu Ludigija ameongezea kuwa ikibainika kama zoezi
hilo lina tija kwa wananchi wa stakishari waliozungukwa na bonde la mto msimbazi
taasisi hizo zikae na wananchi hao na kuwapa maelekezo juu ya umuhimu wa zoezi
hilo ili waweze kuridhika na kutoa maoni yao.
Kwa upande wa
Afisa mazingira Ndug.Shabani Manzi
amesema kuwa kitu kikubwa wanachokifanya ni kuzuia mmomonyoko wa ardhi
na mafuriko kipindi cha mvua, hivyo anaamini zoezi hilo lina tija kwa wanaanchi
wa maeneo hayo.
“Tulikutana na wawakilishi wa wananchi wakatuomba
tuweke kingo katika bonde la mto msimbazi ili kuepuka athari zinazojitokeza
kipindi cha mvua, naamini wananchi wote wanapenda zoezi hilo lifanyike ila
hawapendezwi na namna ya zoezi hilo linavyofanyika hivyo tunawaahidi
tutalifanya zoezi hilo ipasavyo”. Amesema hayo Ndug.Shabani Manzi.
Akiwatoa hofu
wananchi wakazi wa stakishari Ndug. Zakayo Mgaya mmojawapo wa kampuni ya ORAL
INVESTIMENT, amesema kuwa baada ya zoezi hilo kukamilika watahakikisha
wanatengeneza barabara hizo na kuacha mazingira salama.