Na;Rosetha Gange na Judith Damas
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla leo Tarehe 21 Juni 2021 amewaapisha Wakuu
wapya wa Wilaya walioteuliwa tarehe 19 Juni 2021 na Raisi wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika ukumbi wa Arnatoglou
uliopo Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Wakuu Wapya wa Wilaya wakila kiapo Kulia ni Mhe. Kheri Denice James Mkuu mpya wa Wilaya ya Ubungo na kushoto ni Mhe. Fatma Almasi Nyangasa Mkuu mpya wa Wilaya ya Kigamboni |
Hafla hiyo ya uapisho
iliwajumuisha Wakuu wote wa Wilaya tano(5) za Mkoa wa Dar es Salaam,ambapo
Wakuu wa Wilaya wawili ambao ni wapya waliweza kuapa akiwemo Mkuu wa Wilaya ya
Kigamboni Mhe. Fatma Almas Nyangasa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe.Kheri Denice James. Wakuu wa Wilaya Waliosalia hawakuweza kuapa kwa kuwa wawili
walibadilishwa vituo vya kazi akiwemo
aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe ambae sasa ni Mkuu wa Wilaya ya
Temeke Mhe. Jokate Urban Mwegelo na aliyekuwa MKuu wa Wilaya ya Temeke ambaye
sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni
Mhe.Godwin Crydon Gondwe huku Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Ng’wilabuzu
Ndwata Ludigija akibaki katika Wilaya aliyopangiwa awali.
Akizungumza na Wakuu
wa Wilaya Wateule baada ya uapisho Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Amos
Makala alitoa pongezi kwa Wakuu wa Wilaya wapya na kumshukuru Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa uteuzi alioufanya.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla akihutubia |
Aidha, Mhe. Makalla aliweza kuwaelekeza
Wakuu wa Wilaya hao vipaumbele vyake katika utendaji wa kazi ikiwemo ukusanyaji
wa mapato ili Serikali iweze kuwahudumia Wananchi wake na kuleta maendeleo
katika Taifa, usikilizaji na utatuzi wa kero za Wananchi kuanzia Ngazi ya Mtaa
mpaka katika Halmashauri zao,kusimamia ulinzi na usalama kwa kuweka mikakati ya
kudhibiti Uhalifu, kusimamia usafi wa mazingira ili kuweka Mkoa katika hali ya
usfi pamoja na usimamizi,ufuatiliaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.Sambamba na hayo
amesema; “Nendeni mkatimize wajibu wenu ipasavyo na mkatekeleze
matarajio ya Mhe.Rais Samia Suluhu
Hassan kwani amewaamini na ndio maana amewapa nafasi hizo.”
Akitoa neno la Shukurani kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya wengine, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Ng’wilabuzu Ludigija aliahidi kufanya kazi kwa ushirikiano na watendaji wenzake pamoja na kuyapokea maagizo yote yaliyoagizwa na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam vilevile kuyatekeleza majukumu yao yote kwa weledi.