Na: Hashim Jumbe
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekuwa kinara kwenye ukusanyaji wa wingi wa mapato (pato ghafi) ikizipita Halmashauri nyengine 183 nchini, ambapo kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/2022 kuanzia Julai hadi Septemba, 2021 imekusanya Shilingi 17,774,288,777.52/= sawa na 26% ya lengo lake la mwaka ambalo ni Shilingi 69,655,000,000.00/=
Katika taarifa iliyotolewa leo tarehe 28 Oktoba, 2021 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Ummy A. Mwalimu (Mb) imeonesha pia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwenye matumizi ya mapato yake ya ndani ya kwenye miradi ya maendeleo kwa kipindi cha Julai hadi Septemba, 2021 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imetumia Shilingi 5,655,932,578 sawa na 72% kutokea kwenye 60% ya mapato yaliyokusanywa yasiyolindwa ambayo ni Shilingi 7,892,653,225/=
Halkadhalika, kwenye mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa kipindi cha Julai hadi Septemba, 2021 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imetoa mikopo ya Shilingi Bilioni 1.4 ikiwa ni 106% fedha hiyo hutolewa 10% kutokea kwenye mapato yaliyokusanywa yasiyolindwa kwa kipindi cha Julai hadi Septemba, 2021 ambayo ni Shilingi 13,154,422,042.14