DC Ludigija ashiriki zoezi la usafi wa mwisho wa Mwezi Julai

 Katika kutekeleza Kampeni ya Usafi iliyozinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ya ‘Pendezesha Safisha Dar es Salaam’ Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo tarehe 25 Juni, 2022 wamefanya usafi katika kata ya Jangwani ikiwa ni sehemu ya kuendeleza kampeni ya Safisha Pendezesha Dar es Salaam ambapo usafi huo hufanywa kila Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi.

Zoezi hilo la usafi lililoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mheshimiwa Ng’wilabuzu Ludigija liliweza kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Diwani wa Kata ya Jangwani, Jeshi la Zimamoto, Watendaji kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Asasi mbalimbali ikiwemo ‘Juza Waste Pickere Initiative’ Taasisi ya kutokemeza kifua kikuu, pamoja na wananchi wa Kata ya Jangwani wakiongozwa na vijana walioathiriwa na madawa ya kulevya ambao kwasasa wamesaidiwa na Juza Waste Pickers Initiative ambao hujishughulisha na uokotaji wa taka ikiwa ni sehemu ya utunzaji wa mazingira.

Akizungumza katika zoezi hilo Mheshimiwa Ludigija amewata Wananchi kushiriki usafi kama desturi yao na sio kusubiri mpaka mwisho wa mwezi ufike ili kuweka mazingira safi na kuhakikisha Jiji la Dar es Salaam linapendeza na kuwa safi, "Tuhakikishe kwamba usafi ni jambo la kwanza katika Wilaya yetu na ukilinganisha kwamba sisi ni Jiji Lazima tuendane na hadhi ya Jiji letu hivyo nipende kutoa wito kwa Mtendaji wa Kata ya Jangwani kuhakikish kua anashirikiana na  viongozi pamoja na wadau  wengine kuwatumia vijana wa kata hii kuokota taka Lengo likiwa ni kupendezesha Jiji na kutekeza kampeni yetu ya Safisha Pendezesha Dar es Salaam hivyo tuufanye usafi kama desturi yetu na tusisubiri hadi mwisho wa mwezi ufike."


Sambamba na hilo Mheshimiwa Ludigija ameweza kuzindua Asasi ya utunzaji wa Mazingira maarufu kama ‘Juza Waste Pickers Initiative’ ambayo ilianza mwaka 2012 kama kikundi kidogo cha waokota taka wakisaidiwa na vijana walioathiriwa na madawa ya kulevya ambapo hadi kufikia Aprili, 2022 Juza Waste Pickers Initiative kusajiliwa rasmi na kua Asasi ya Utunzaji wa Mazingira, aidha Asasi hiyo imekua ikishirikiana na vijana hao kwa ukaribu zaidi lengo likiwa ni kuwawezesha vijana kiuchumi na pia kuwafanya waondokane na matumizi ya madawa ya kulevya na kurudi katika hali zao za kawaida."Amesema Mheshimiwa Ludigija.

"Niwapongeze kwa jambo hili zuri la kuwasaidia vijana wetu kuondokana na wimbi la uvutaji madawa ya kulevya na kuamua kuwaajiri katika kazi ya kutunza mazingira ambapo hadi sasa wamekua wakijali afya zao hivyo kuamua kutoa bima za afya  kwa vijana 30 Lengo likiwa ni kuhakikisha wanaimarisha afya za vijana hao, hivyo niwakaribishe wadau wengine watakaowiwa katika hili lengo likiwa ni kumuunga mkono Mheshimowa Raisi katika kuimarisha sekta ya Afya.

Kwa upande mwingine Mheshimiwa Ludigija amewasisitiza wananchi kushiriki vyema katika zoezi la Anuani za Makazi ambapo amewaagiza kuhakikisha wanaweka namba kwenye nyumba zao pamoja na vibao vya mitaa  lengo likiwa ni kurahisisha mawasiliano majanga yanapotokea na pia kuimarisha biashara zao lakini pia zoezi hilo la Anuani za Makazi litarahisisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 inayotarajiwa kufanyika  mwezi wa Nane mawaka huu.

 

"Natoa Wito kwa viongozi wa Kata wakiongozwa na Madiwani husika kuhakikisha wanasimamia vizuri zoezi la Anuani za makazi kwa kuhakikisha Mitaa yote inakua na vibao pamoja na nyumba zote kua na Namba hivyo niwaombe wananchi kushiriki vizuri kwa kuhakikisha nyumba zao zina namba.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi