RC Chalamila amtaka mkandarasi kukamilisha ujenzi wa Machinjio ya Vingunguti kwa wakati

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila amemtaka mkandarasi anayesimamia mradi wa machinjio ya kisasa ya Vingunguti kukamilisha mradi huo kwa wakati uliopangwa. Hayo yameelezwa leo Desemba 22, 2023 Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kukagua machinjio hiyo.



Akizungumza wakati wa ukaguzi wa machinjio hiyo Mhe. Chalamila amesema “Kipekee namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa pesa kiasi cha Billioni 8 kwaajili ya machinjio hii, lakini pia niwashukuru Mkuu wa Wiaya na Mkurugenzi wa Jiji kwa kusimamia mradi. Mradi huu wa machinjio ni mradi wa kisasa na ni miongoni mwa machinjo bora nchini, hivyo nimtake mkandarasi Shirika la Nyumba kukamilisha yale maeneo ambayo hayajakamilika ili wananchi wa Vingunguti waweze kuendesha shughuli zao za kiuchumi na Halmashauri kuongeza mapato na kuhakikisha malengo ya Serikali ya kuanzisha mradi huu yaweze kutimia."

Aidha, amemuagiza Mkuu wa Wilaya kuunda kamati maalumu itakayochunguza mwenendo wa utendaji kazi katika machinjio hiyo ili kubaini changamoto zilizopo na kutoa mapendekezo ya Mambo ya kufanya ili kuboresha shughuli zinazoendelea machinjioni hapo.



Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo ametoa shukrani zake kwa Mkuu wa Mkoa kwa ziara anazoendelea kufanya za kukagua Miradi ya Maendeleo pamoja na kuongea na wananchi huku akimuhakikishia kutekeleza yote aliyoyaagiza.



Machinjio hiyo ambayo imejengwa kwa kiasi Cha shilingi Bilioni 12, ikiwa ni Fedha kutoka Mapato ya Ndani ya Halmashauri na Fedha kutoka Serikali Kuu na inatarajiwa kuwa msaada mkubwa kwa wafanyabiashara wa nyama kutoka ndani ya nchi na wale wa nchi jirani.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi