Miradi ya Bilioni 40.9 yamulikwa na Mwenge wa Uhuru 2024 Wilaya ya Ilala, Mkurugenzi Satura awapongeza Watumishi wake

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Ndugu Jomaary Mrisho Satura ametoa salamu za pongezi kwa Watumishi wake kufuatia ushiriki wao kwenye Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024, ambapo Mwenge wa Uhuru umepita kwenye miradi (07) na kupokea taarifa ya miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru 2023.  

Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 ukizindua mradi wa Kituo cha Polisi - Mwanagati, tarehe 8 Mei, 2024

Akitoa salamu hizo, Mkurugenzi Satura alisema "Ndugu zangu, kwa dhati kabisa ya moyo nawashukuru sana kwa namna ambavyo tumeshiriki kikamilifu kwenye maandalizi na kisha kuukimbiza Mwenge wetu wa Uhuru 2024 katika miradi yetu yote (7) ndani ya Jiji letu la Dar es salaam na kufanikiwa kuvuka salama"

Mwenge wa Uhuru 2024 ukikagua na kutembelea Mradi wa Usambazaji Maji kusini mwa Mkoa wa Dar es Salaam, tarehe 8 Mei, 2024

Kwenye salamu zake Mkurugenzi Satura ameeleza hisia zake kwa Watumishi kua "Najisikia fahari kubwa sana kufanya kazi nanyi, naomba 'spirit' hii na 'team work' hii iendelee na kuwa utamaduni wetu wa ufanyaji kazi kila siku na kila mahala"

Aidha, Mkurugenzi Satura alisisitiza kuwa "Nikiwa nafahamu ya kuwa kazi ilikuwa nzito na ngumu na 'probably' mmechoka sana, niwaombe asubuhi hii kwa pamoja tujitahidi kuendelea kuwa na ari na nguvu ili tuweze kuusindikiza Mwenge wetu na kuukabidhi kwa wenzetu wa Wilaya ya Temeke" 

Moja ya Jengo kwenye Kituo cha Afya Kinyerezi, lililozinduliwa na Mwenge wa Uhuru, tarehe 8 Mei, 2024

Mwisho Mkurugenzi Satura alimalizia kwa kusema "Desturi yangu, kama navyopenda kukemea yasiyofaa kufanywa ndivyo nilivyo mwepesi kupongeza mazuri yanayofanywa. Tufanye mazuri ili kudumisha na kuendeleza mahusiano na upendo wa kweli. Kurugenzi ni Taasisi bila ya ninyi, Mimi siyo lolote wala chochote 'Nawapenda sana ndugu zangu''

Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 Godfrey Mnzava akipanda mti kwenye Shule ya Sekondari Minazi Mirefu, kwenye halfa ya ukaguzi na utiaji wa jiwe la msingi, tarehe 8 Mei, 2024


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi