Mkurugenzi Jiji la DSM awapongeza Watumishi kwa kushiriki Mwenge wa Uhuru 2024 kikamilifu

Ndugu zangu, kwa dhati kabisa ya moyo nawashukuru sana kwa namna ambavyo tumeshiriki kikamilifu kwenye maandalizi na kisha kuukimbiza mwenge wetu wa Uhuru 2024 katika miradi yetu yote 7 ndani ya Jiji letu la Dar es salaam na kufanikiwa kuvuka salama. 

Uzinduzi wa Mradi wa Kituo cha Polisi - Mwanagati

Najisikia FAHARI kubwa sana kufanya kazi nanyi, naomba SPIRIT hii na TEAM WORK hii iendelee na kuwa UTAMADUNI wetu wa ufanyaji kazi kila siku na kila mahala.

Mwenge wa Uhuru ukitembelea Mradi wa Usambazaji Maji kusini mwa Mkoa wa Dar es Salaam, uliopo Bangulo, Kata ya Pugu Stesheni

Nikiwa nafahamu ya kuwa kazi ilikuwa nzito na ngumu na probably mmechoka sana, niwaombe asubuhi hii kwa pamoja tujitahidi kuendelea kuwa na ARI na NGUVU ili tuweze kuusindikiza mwenge wetu na kuukabidhi kwa wenzetu TEMEKE 

Jengo la Wazazi kwenye Kituo cha Afya Kinyerezi, mradi ambao umezindulia na Mwenge wa Uhuru 2024 Mei 8, 2024


Desturi yangu, kama navyopenda kukemea yasiyofaa kufanywa- ndivyo nilivyo mwepesi kupongeza mazuri yanayofanywa. Tufanye mazuri ili kudumisha na kuendeleza mahusiano na upendo wa kweli

Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 Godfrey Mnzava akipanda mti kwenye Shule ya Sekondari Minazi Mirefu, ikiwa ni mmoja wa mradi uliowekewa jiwe la msingi na Mwenge wa Uhuru 2024

Kurugenzi ni TAASISI bila ya ninyi, mimi SIO LOLOTE WALA CHOCHOTE - NAWAPENDA SANA NDUGU ZANGU

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi