Jiji la DSM lafanya Usafi wa Mazingira kuelekea Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo leo tarehe 24 Aprili, 2024 ameongoza shughuli za Usafi wa Mazingira katika eneo la Barabara za Lumumba na Nkurumah ikiwa ni zoezi maalum kuelekea siku ya Kihistoria, siku ya Miaka 60 ya Jamuhuri ya Muungano Tanzania.


Akiongoza Mhe. Edward Mpogolo amewashukuru viongozi wa Serikali za Mitaa na Kata, makampuni ya usafi pamoja na wananchi kwa kushiri

Sisi kama Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam tunashirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha barabara hizi zinakua katika hali safi na bora kwani Dar es Salaam hususani Wilaya ya Ilala Ndio Kitovu cha kupokea wageni wanaoingia nchini hivyo tuweke mazingira yetu katika hali ya usafi wakati wote ili pindi wageni wetu wanapofika wajivunie mazingira ya Nchi yetu yanavyopendeza na kuvutia yakiwa katika hali ya usafi. Pia tumeshawaagiza wamiliki wa makampuni yaliyoko pembezoni mwa barabara kutoka Airport hadi mjini kupanda miti iloyorafiki huku tukiwataka wamiliki wa nyumba zilizoko katikati ya mji kuhakikisha wanapaka majengo yao rangi lengo likiwa ni kuendelea kulipendesha Jiji letu.” Amesema Mhe. Mpogolo.


Sambamba na hilo Mhe. Mpogolo ameelndelea kusema “Sisi kama Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam tumeshikamana na tumeimarika kwa Maendeleo ya Nchi kwani ndani ya miaka 60 ya Muungano tumeweza kutumia fedha za mapato ya ndani kupendezesha Jiji letu kwa kuweka vitofali (pavements) barabara zetu za mjini hivyo, niwaombe wakandarasi wa makampuni kuhakikisha mnashirikiana na uongozi wa Jiji kwa ukaribu zaidi katika kuhakikisha zoezi la usafi linakua kipaumbele ili tuepukane na magonjwa ya mlipuko hasa kipindi hichi cha mvua.


Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Taka Ngumu na Usafishaji Rajabu Ngoda ameeleza kuwa matukio haya yanayofanywa na Jiji la Dar es Salaam kuelekea sherehe za Muungano yamekua chachu ya kuleta mafanikio zaidi kwa Jiji la Dar es Salaam kuwa Safi kwani wananchi wameonekana kujitokeza kwa wingi katika zoezi la usafi huku akimuhakikishia Mkuu wa Wilaya ya Ilala kutekeleza yale yote aliyoyaelekeza na kusema Jiji la Dar es Salaam litazidi kuimarika na kushikamana kufanya usafi kwa afya za wananchi wake.


Naye Mkandarasi kutoka Kajenjere Trading Company Limited,  Matthew Andrew ameeleza kuwa pamoja na changamoto wanazokutana nazo wakati wa kufanya usafi, atahakikisha kushirikiana na viongozi na wataalamu wa Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha Jiji linakua safi kwa ustawi wa afya za wananchi na Taifa kwa ujumla.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi