Shule ya Sekondari Kinyerezi yapokea samani kutoka Hazina SACCOS

Shule ya Sekondari Kinyerezi leo Mei 20, 2024 imepokea msaada wa samani (viti vya walimu, meza ya Mkuu wa Shule pamoja na kabati la kutunzia nyaraka) kutoka kwa chama cha ushirika wa akiba na mikopo Hazina SACCOS 


Akipokea msaada huo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Hazina SACCOS, Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Liberia Minja amewashukuru wadau hao wa elimu kwa uamuzi wao wa kuisaidia Serikali kutatua changamoto katika utoaji wa huduma za jamii na kwamba Serikali inathamini jitihada hizo.


"Samani hizi zimekuja wakati ambao Serikali ya awamu ya sita inasisitiza ubora wa miundombinu ya elimu kwa lengo la kukuza ujuzi katika kufundisha. Nawashukuru sana Hazina SACCOS kwa msaada huu na wasichoke kutoa pale ambapo tutakuja tena." Amesema Mwl. Minja


Nae Mtendaji Mkuu wa Hazina SACCOS Festo Mwaipaja amesema msaada huo walioutoa ni sehemu ya utaratibu wao wa kurudisha kwa jamii na utasaidia kuondoa dosari ya upungufu wa viti na meza za walimu.


Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Kinyerezi Mwl. Daniel Mwakyambiki ametoa shukrani kwa Hazina SACCOS kwa msaada huo kwani utasaidia walimu kufundisha katika mazingira rafiki na kufaulisha wanafunzi na kutoa wito kwa walimu kutunza vizuri samani hizo ili zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi