Jiji la DSM Laweka Mikakati ya Kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam yaweka mikakati madhubuti ya kushinda Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) yanayotarajiwa kuanza Mei 27, 2024 Dar es Salaam kwa ngazi ya Mkoa , hayo ameyabainisha leo na Mratibu wa Michezo UMITASHUMTA Jiji la Dar es Salaam Mwl. Charles Ndilime wakati wakiendelea na mazoezi ya kujifua kisawasawa kwaajili ya mashindano hayo kwenye kambi ya Chuo cha Urekebishaji Tabia, Ukonga Jijini Dar es Salaam.


Aidha Mwl. Ndilime ameeleza kuwa “Baada ya kumaliza mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya klasta tumetengeneza timu ya Wilaya ya Ilala ambayo ina siku nne kambini kwaajili ya kujiandaa na mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa yanayoyotarajiwa kuanza Mei 27, 2024 katika viwanja vya Chuo cha Ualimu DUCE pamoja na Shule ya Sekondari Jitegemee hivyo niwahakikishie tutarudi na ushindi mnono na matarajio yetu ni kurudisha tena kombe la jumla ambalo tumeshachukua mara tano mfululizo kwani vijana wetu wana morali na tunaamini hawatatuangusha".


Sambamba na hilo Mwl. Ndilime ameeleza kuwa michezo inayoshindaniwa ni pamoja na mpira wa miguu kwa wasichana na wavulana, mpira wa pete, Mpira wa kengele kwa wasichana na wavulana, Mpira wa wavu kwa wasichana na wavulana, mpira wa mikono kwa wasichana na wavulana, Riadha pamoja na Fani za ndani (kwaya, ngoma, na muziki) ambapo Jumla ya wanamichezo ni 120, na kati ya hao Wavulana ni 63 na Wasichana ni 57.


Aidha, Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Mei 27 -30, 2024 kwa ngazi ya Mkoa sambamba na kauli mbiu isemayo ‘Miaka 60 ya UMITASHUMTA tunajivunia mafanikio katika sekta ya Elimu, michezo na sanaa, Hima Mtanzania shiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024.’


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi