Wakazi wa Gongolamboto wahimizwa uzingatiaji wa lishe bora kwa mama wajawazito na watoto wa umri chini ya miaka mitano

Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam kupitia Idara ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii imetoa elimu juu ya kuzingatia lishe kwa kina mama wajawazito katika Zahanati ya Gongolamboto.


Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu hiyo, Afisa Lishe wa Jiji la DSM Bi. Neema Mwakasege amesema kuwa lishe ni muhimu kwa kina mama hasa wajawazito sababu wanapokua katika hali hii wanahitaji madini mengi mwilini hivyo ni muhimu kuzingatia.


Naye Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Gongolamboto Dkt. Besta Benedicto Sanga amesema anashukuru kwa elimu hiyo endelevu kutoka Jiji la Dar Es Salaam kupitia Jiko Darasa kwa wajawazito na kuwashukuru waliojiotokeza na na kusisitiza kuzingatia yale wanayoelekezwa na wataalamu.


Ikumbukwe kuwa ajenda hii ya lishe ni moja kati ya mipango endelevu ndani ya Jiji la Dar Es Salaam na Taifa kwa ujumla hivyo ni muhimu kila mwananchi kuzingatia lishe bora kwa Ustawi wa Jamii.



Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi