Wakazi wa Jiji la DSM wahimizwa uzingatiaji wa lishe kwa mama wajawazito

Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam kupitia Idara ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii imetoa elimu juu ya kuzingatia lishe kwa kina mama wajawazito katika Zahanati ya Vingunguti iliyobeba kaulimbiu isemayo '𝙇𝙞𝙨𝙝𝙚 𝙗𝙤𝙧𝙖 𝙠𝙬𝙖 𝙗𝙖𝙗𝙖, 𝙢𝙖𝙢𝙖 𝙣𝙖 𝙢𝙩𝙤𝙩𝙤 𝙣𝙞 𝙢𝙨𝙞𝙣𝙜𝙞 𝙬𝙖 𝙟𝙖𝙢𝙞𝙞 𝙗𝙤𝙧𝙖 𝙣𝙖 𝙏𝙖𝙞𝙛𝙖 𝙚𝙣𝙙𝙚𝙡𝙚𝙫𝙪'


Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu hiyo, Afisa Lishe wa Jiji la DSM Bi. Neema Mwakasege amesema kuwa lishe ni muhimu kwa kina mama hasa wajawazito sababu wanapokua katika hali hiyo wanahitaji madini mengi mwilini.


Naye Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Vingunguti Dkt. Isaack Makundi amesema anashukuru kwa elimu hiyo endelevu kutoka kwa wataalamu wa lishe wa Jiji la Dar es Salaam kupitia Jiko Darasa kwa wajawazito, na kuwashukuru waliojiotokeza na kusisitiza kuzingatia yale wanayoelekezwa na wataalamu.


Ikumbukwe kuwa ajenda hii ya lishe ni moja kati ya mipango endelevu ndani ya Jiji la Dar Es Salaam na Taifa kwa ujumla hivyo ni muhimu kila mwananchi kuzingatia lishe bora kwa Ustawi wa Jamii.




Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi