RC Chalamila atembelea banda la Machinga Complex kwenye Maonesho ya Nanenane

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila leo tarehe 07 Agosti, 2024 ametembelea banda la Machinga Complex kwenye maonesho ya wakulima na wafugaji yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwl. Nyerere Mkoani Morogoro kwa Kanda ya Mashariki.


Akizungumza na wajasiliamali hao, Mhe. Chalamila amewaasa kutengeneza bidhaa zenye ubora ili kupata soko la uhakika na kujiongezea mapato ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla wake na kueleza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan iko pamoja katika kuwatafutia mitaji ya biashara na kuweka mazingira mazuri yakufanya biashara zao. 


Aidha, Mhe. Chalamila ametoa pongezi kwa wajasiriamali hao kwa kujituma na kushiriki kwenye maonesho hayo kwani ni hatua muhimu katika kujitangaza na kupata masoko ya uhakika.


Kaulimbiu ya maadhimisho ya Nanenane kwa mwaka 2024 inasema "Chagua viongozi bora wa Serikali za Mitaa kwa maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi".


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi