DC Mpogolo atembelea banda la Jiji la DSM kwenye Maonesho ya Nanenane

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo leo tarehe 06 Agosti, 2024 ametembelea banda la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwenye maonesho ya wakulima na wafugaji yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwl. Nyerere Mkoani Morogoro kwa Kanda ya Mashariki.


Akizungumza mara baada ya kutembelea Banda hilo, Mhe. Mpogolo amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la DSM na timu yake kwa maandalizi mazuri ya uandaaji wa maonesho kwani kuna utofauti mkubwa unaonekana kulinganisha na miaka iliyopita.


Halmashauri ya Jiji la DSM tumeitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuzitaka Halmashauri zote Tanzania Kutoa Elimu kwa wananchi kwenye masuala ya kulimo, ufugaji na uvuvi. Katika maonesho haya tumeona jinsi hata mwenye eneo dogo anaweza kupanda bustani ya mbogamboga zitakazoweza kusaidia katika suala zima la lishe bira kwa familia." Amesema Mhe. Mpogolo.


Aidha, ametoa wito kwa wananchi wa Morogoro na wanaotoka kanda ya mashariki kutembelea banda la Halmashauri ya Jiji la DSM kujifunza kilimo na ufugaji kwani kuna watalamu waliobobea.


Sambamba na hilo, Mhe. Mpogolo amesema “Kulingana na kaulimbiu ya Nane Nane 2024 inayosema 'Chagua viongozi bora wa Serikali za Mtaa kwa maendeleo endelevu ya kilimo, mifugo na uvuvi' nitumie nafasi hii kuwaasa wananchi wa Ilala kujiandikisha kwenye daftari la kudumu katika mitaa yetu na pindi muda utakapofika wa kupiga kura tukachague viongozi bora watakao watumikia wananchi ili kuleta maendeleo katika jamii.



Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi