DC Mpogolo atoa wiki mbili kwa DAWASA kudhibiti mfumo wa maji taka Buguruni

MKUU wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo, ametoa wiki mbili kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kudhibiti kuvuja kwa kinyesi katika mfumo wa maji taka katika Mtaa wa Kisiwani, Buguruni, jijini Dar es Salaam.


Mhe. Mpogolo ametoa maagizo hayo leo Septemba 3, 2024 wakati wa ukaguzi katika eneo hilo kutokana na malalamiko ya wananchi kuhusu DAWASA baada ya chemba za mfumo huo kufurika kinyesi na kuleta adha kubwa.


Aidha, amegiza mamlaka hiyo, kufumua mfumo huo baada ya kubaini umejengwa chini ya kiwango.

Natoa wiki mbili kwa DAWASA , kurekebisha mfumo huu wa majitaka. Dhamira ya serikali yetu chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kujenga mradi huu siyo kuwaletea adha wananchi bali ni kuwaondolea kero.” amesema Mhe. Mpogolo.


Aidha, amesema amezungumza na Mkrugenzi Mtendaji wa DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire, kufika katika eneo hillo kuukagua mradi huo na kujiridhisha juu ya ubora wake.


Bwire atakuja hapa kesho akague mradi huu na kujionea hali hii. Pia aangalie ubora wa mradi . Najua ni msikivu na ni mtendaji mzuri.”amesema.

Aidha, amesema miongoni mwa changamoto alizobaini katika mradi huo ni kujengwa kwa kiwango cha chini, ikiwa ni pamoja na mabomba madogo ya kupitisha maji taka yasiyoendana na wingi wa wakazi wa eneo hilo.


Mkuu wa Wilaya huyo, alionya vikali wananchi kutupa taka ngumu katika chemba za mradi huo hali inayosabababisha kuziba na kuvujisha maji taka.

Kwa upande wake Afisa wa DAWASA, Charles Makoye, aliwaomba radhi wananchi wa eneo hilo, huku akieleza chanzo ni baadhi ya wananchi hao kutupa taka ngumu katika mfumo huo.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi