Madiwani na Wataalamu kutoka Nchini Kenya Wafanya ziara ya Mafunzo Jijini DSM

Halmashauri ya jiji la Dar es salaam leo tarehe 26 Agosti, 2024 wamepokea Ujumbe wa viongozi na wataalam kutoka Jimbo la kilifi Nchini Kenya waliofika kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu katika eneo la ukusanyaji wa mapato pamoja na utekelezaji wa miradi.


Wakiwa katika Ukumbi wa Mikutano wa Arnatoglou Jijini humo, Wataalumu hao waliweza kujifunza namna mbalilimbali Jiji la Dar es Salaam linavyofanya kazi zake katika eneo la ukusanyaji wa mapato pamoja na kujifunza mbinu mbalimbali za kuongeza mapato pamoja na kusimamia miradi kwani kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam mapato yameongezeka kwa kasi kutokana na kuanzishwa kwa kanda za huduma ambazo zimekua chachu ya ongezeko la asimia 105% ya mapato ya ndani ya Halmashauri ukilinganisha na mwaka 2022/2023 .


Sambamba na hilo Waheshimiwa hao Waliweza kujifunza mbinu mbalimbali za uwekezaji ambapo kwa Jiji la Dar es Salaam wamewekeza kwenye masoko kwani kuna mpango wa ujenzi wa masoko ya kisasa matatu ambayo yatakua Chachu ya kuongeza mapato kwa Jiji kwani muundo wa ujenzi wa masoko hayo ni rafiki na utakua na eneo la maegesho la kulipia hivyo kupitia maegesho hayo Halmashauri pia itapata mapato zaidi.


Akiongea wakati wa Mafunzo, hayo Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Ndg. Elihuruma Mabelya ameeleza kuwa “Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekua mstari wa mbele kuhimiza ushirikiano na mahusiano mazuri na nchi za jirani, hivyo nitumie nafasi hii kuwakaribisha sana katika jiji letu, Tubadilishane mawazo na mbinu mbalimbali kwa maslahi ya wananchi wetu tunaowaongoza . Mafanikio haya tunayoyapata yanatokana na juhudi, bidii pamoja na mshikamano kati ya madiwani wetu na wataalamu. hivyo niwaombe Madiwani kutoka Kilifi mkatekeleze vyote mlivyojifunza bila kusahau ushirikiano na watalamu kwani wao ndio watendaji wakuu”.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati wa Fedha na Mipango ambaye ni mwakilishi wa Wadi ya Kaloleni Jimbo la Kilifi Mhe. Birya Fondo amempongeza Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam pamoja na watendaji wote kwa kuweza kushirikiana vyema katika kukuza mapato ya Jiji pamoja na usimamizi na utekelezaji mzuri wa miradi huku akiahidi kwenda kufanyia kazi yote waliyojifunza.


Kipekee naomba kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa mapokezi mazuri kutoka kwenu na pia kujitoa kwenu kutupatia Elimu hii ya ukusanyaji wa kodi na utekelezaji wa Miradi , Hakika ziara yetu imekua yenye mafanikio makubwa kwani tumejifunza mambo mengi na mazuri na tutayafanyia kazi pindi tutakaporejea Kilifi “ Amesema Mhe. Birya


Aidha, Madiwani na watalamu hao Waliweza kutembelea Soko la Kimataifa la Samaki Feri pamoja na Soko la Kisutu kujifunza namna Jiji la Dar es Salaam linavyoendesha masoko hayo katika kuhakikisha mapato yanaongezeka.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi