MANISPAA YA ILALA NA WWF WAPANDA MAJANI KUZUIA MMOMONYOKO WA UDONGO KWENYE KINGO ZA MTO MSIMBAZI

Na: Hashim Jumbe
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na Shirika la Mazingira Duniani la ‘World Wide Fund for Nature’ (WWF) limepanda majani aina ya vetiva kwenye kingo za mto Msimbazi ili kuzuia athari za mmomonyoko wa udongo zinazoweza kusababishwa na kasi kubwa ya maji yanayotiririka katika mto huo hususani katika vipindi vya mvua.

Zoezi hilo la upandaji majani katika kingo za mto Msimbazi, limefanyika katika eneo la Msewe Liwiti kata ya Segerea na inatarajiwa kupandwa majani katika eneo lenye urefu wa kilomita 25 kwenye kingo za mto Msimbazi.

Majani hayo yanatabia ya kunyonya sumu kwenye ardhi, pia yatazuia muendelezo wa mmomonyoko wa kingo kwenye mto Msimbazi na kupunguza hewa chafu katika maeneo hayo.

Mratibu wa Mradi wa Nishati na Mazingira ‘WWF’ kutoka Tanzania Dr. Teresia Olemako wa pili kutoka kulia, akipanda majani aina ya vetiva kwenye kingo za mto Msimbazi kuzuia athari za mmomonyoko wa udongo



Muwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Ndugu Charles Secha akipanda majani katika kingo za mto Msimbazi eneo la Misewe kata ya Segerea


Maafisa Mazingira wa Manispaa ya Ilala wakishiriki zoezi la upandaji majani aina ya vetiva kwenye kingo za mto Msimbazi

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi