Waziri Kairuki akagua Miradi ya Maendeleo Jimbo la Segerea

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. Angellah Kairuki ametoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha kuwa ndani ya Siku Saba wanafuatilia eneo kwa ajili ya ujenzi wa Shule nyingine mpya ya Msingi ya Kifuru, Walimu wanapata Viti na Meza pamoja na madawati 500 yawe yamefika katika Shule hiyo.


Sambamba na hili pia amemuelekeza Mhandisi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha ndani ya Mwezi Mmoja Shule iweimepata matundu 20 ya vyoo.

Mhe. Kairuki ametoa maelekezo hayo leo Machi 1, 2023 wakati alipofanya ziara yake katika Jimbo la Segerea, lengo likiwa ni kukagua miradi ya maendeleo hususani kwenye Sekta yaAfya, Elimu na Miundombinu ya Barabara


Aidha, Mhe. Kairuki ameendelea kuelekeza alipotembelea Shule ya Msingi Ari kuwa tathmini na chuo cha DIT ifanyike mapema kwa ajili ya ujenzi wa Ghorofa 3 ambapo ghorofa ya chini imeshaanza katika Shule hiyo ya Sekondari “Chuo cha DIT siyo mbali na kipo Dar es Salaam hivyo tathmini ifanyike mapema na tathmini hiyo itatusaidia kuendelea na Ujenzi wa Ghorofa 3 ambapo ghorofa ya chini imeshaanza katika Shule ya Sekondari Ari" Amesema Mhe. Kairuki.


Aidha, Mhe. Kairuki alitembelea Shule ya Sekondari Kisungu ambayo ilipata mradi wa madarasa nane (8) kwa Shilingi milioni 160 ambazo ni fedha za UVIKO-19 na mradi wa ujenzi wa madarasa 14 ulipokea kiasi cha Shlingi Milioni 280 kutoka katika mfuko wa Pochi la Mama ambapo mpaka sasa Shule ina vyumba vya madarasa ishirini na nane (28) na Maabara mbili (2).


Akiendelea na ziara hiyo katika Zahanati ya Bonyokwa Mhe. Kairuki amesema kuwa k atika Mradi wa DMDP awamu ya pili wataanzia na barabara inayoenda Zahanati ya Bonyokwa ambayo imetengewa kiasi cha Shilingi Bilioni 3.5 kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo, ameongeza kuwa zaidi ya miradi 35 imeteekezwa katika Jimbo hilo la Segerea. Pia ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kutenga kiasi cha Bil. 6 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ndani ya Jimbo la Segerea sambasamba na hilo kiasi cha Sh. Mil 140 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kimanga.

Pamoja na miradi hiyo, lakini pia Mhe. Kairuki ametembelea eneo la wazi lililopo kata ya Bonyokwa ambalo linatarajiwa kujengwa Stendi na Soko ambapo pia ameiagiza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia mapato yake ya ndani kuhakikisha wanajenga Soko na Stendi hiyo ”Maafisa Mipango Miji na Mthamini waje nakupitia, Mkae vizuri na kufanya tathimini na utafiti wakina, ulipaji wa fidia ukamilike na msichukue muda mrefu. Pia kufata muongozo, kuzingatia Sheria, thamani ya fedha na muda pia.”


Pia Mhe.Kairuki amempongeza Meya wa Jiji la Dar es Salaam kwa kutenga bajeti ya mwaka 2023/2024 katika kutekeleza miundombinu mbalimbali, vilevile Halmashauri hiyo kupitia mapato yake ya ndani imetenga kiasi cha Shilingi Milioni 575 kwaajili ya ujenzi wa Kivuko katika eneo lililopo Kata ya Kimanga na kutoa wito kwa wanachi wa Jimbo la Segerea kuhakikisha wanalipa mapato kwa wakati na wasilalamike juu ya tozo kwani fedha hizo ndiyo msaada mkubwa wa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika nchi yetu.

Naye Mbunge wa Jimbo la Segerea Mhe. Bonnah Kamoli amemshukuru Mhe. Kairuki kutoa muda wake kwa kufanya ziara katika Jimbo lake huku akisikiliza na kutoa maelekezo ya kutekelezwa miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo katika Sekta ya Afya, Elimu na barabara.


Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Ilala Bi. Charangwa Makwiro naye amems hukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwakujali wananchi, kwa upande wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ilipokea fedha nyingi zaidi katika kutekeleza Miradi ya Maendeleo kwa upande wa ujenzi wa madarasa ilipokea kiasi cha Shilingi Bilioni 6.2 fedha maarufu kama “Pochi la Mama” kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa 310 hivyo Tunatoa shukrani zetu kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya yakutuletea miundombinu na kutusogezea huduma za kijamii karibu.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi