Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii Jiji la DSM yakagua miradi iliyotekelezwa kwa kipindi cha robo ya tatu Januari - Machi, 2023

Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, leo tarehe 8 Mei, 2023 imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2022 /2023 ulioanza Januari hadi Machi 2023.


Aidha Kamati iliweza kutembelea na kukagua miradi mitatu, ambapo mradi mmoja ni moja ya miradi itakayotembelewa na Mbio za Mwenge wa Uhuru ikiwa ni ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Zingiziwa, huku miradi mingine miwili ikiwa ni ujenzi wa madarasa 20 ya ghorofa katika Shule ya Sekondari Amani pamoja na ujenzi wa jengo la Maktaba pamoja na Ukumbi katika Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa.


Aidha, ujenzi wa Kituo cha Afya Zingiziwa uliogharimu shilingi Milioni 500 zikiwa ni Fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri, umekamilika kwa asilimia 99 na hadi kufikia Mei 30, 2023 ujenzi utakua umekamilika kwa asilimia mia moja. Pia ujenzi wa Madarasa 20 ya ghorofa Shule ya Sekondari Amani ulioanza Juni, 2022 na hadi kufikia 30, Agosti mradi huo wenye thamani ya shilingi Bilioni 1.6 utakua umekamilika huku ujenzi wa jengo la maktaba pamoja na Ukumbi katika Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa ukiwa hatua ya Jamvi ambapo hadi kufikia Novemba 2023 ujenzi huo uliogharimu shilingi bilioni 1.2 unatarajiwa kukamilika.


Akifanya majumuisho ya ziara hiyo Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Robert Manangwa amesema, "Leo tumetembelea baadhi ya miradi inayosimamiwa na kutekelezwa na Halmashauri ya Jiji la DSM ambapo tumeweza kuridhishwa na utekelezaji huo japo kuna marekebisho madogomadogo yakukamilisha hususani katika Kituo cha Afya Zingiziwa hivyo marekebisho hayo inabidi yaboreshwe mapema kabla Mwenge wa Uhuru haujapita kukagua.


Lakini pia niseme Ziara yetu imekua na mafanikio na nawashukuru Wakuu wa Idara wote pamoja na Madiwani kwa kuweza kuitekeleza ziara hii zaidi ya hayo naomba mapungufu yaliyoonekana kwenye miradi hiyo yashughulikiwe kwa wakati na kuweza kufikia hitimisho sahihi kwani lengo la miradi hii ni kwaajili ya Wananchi wetu kupata huduma muhimu na bora kwa wakati.


Aidha kamati imeridhia kuwa miradi yote inayotekelezwa ifuatiliwe kwa ukaribuzaidi ili ikamilike kwa wakati uliopangwa

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi