Kamati ya Mipango Miji na Mazingira ya
Manispaa ya Ilala, imefanya ziara ya kushtukiza katika maeneo korofi yenye
uchafuzi mkubwa wa mazingira, Kamati ilitembelea eneo la Vingunguti kwenye mabwawa
ya maji taka mtaa wa Spenko, na kubaini uchafuzi mkubwa wa mazingira
unaohatarisha afya na maisha ya wakazi wa eneo hilo, mfumo mbovu wa
utiririshaji maji taka yasiyokua na tiba unaofanywa na viwanda vya Sadolini na
Murzah.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji na
Mazingira, Mh. Sultan Salim, akiongea na Blogg yetu alisema ‘‘tatizo la
kutiririsha maji kwenye makazi ya wananchi ni kubwa, hivyo ameomba utafiti wa
kina ufanywe kudhibiti hali hii’’
Kinyume na utaratibu
unavyoelekeza,viwanda hivyo vinatiririsha maji bila kuyatibu na hivyo
kuhatarisha maisha ya wakazi wa eneo lote linalopitiwa na maji hayo ambapo
imeelezwa kuwa watu pamoja na wanyama wanaofugwa majumbani kwa namna tofauti
wameweza kuathirika na maji hayo
Eneo
la kuhifadhi maji taka la Spenko, hapa ndipo maji taka yanapata tiba na baadae
kuyaruhusu kwenda mto Msimbazi, Viwanda vya Murzah na Sadolini wanakwepa
gharama za kuyafikisha maji taka wanayoyatengeneza na badala yake wameweka
mfumo wao usio rasmi na unaoleta athari kwa wananchi
Mfumo
usio rasmi wa umwagaji taka kutoka katika viwanda vya Murzah na Sadolini, maji
taka hayo hayajapatiwa tiba na
yanakwenda moja kwa moja kwenye mto msimbazi,hivyo huathiri viumbe hai
vinavyopatikana kwenye mto huo.
Kamati ya Mipango Miji na Mazingira ya
Manispaa ya Ilala, ilifika katika eneo la kiwanda cha Sadolini na kufanya
ukaguzi wa Mazingira ya ufanyaji kazi na mfumo mzima wa utoaji maji taka,
lakini haikua rahisi kupata idhini ya kufanya ziara.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Sadolini akitoa masharti ya kukaguliwa na Kamati ya Mazingira |
Baada
ya vuta n’kuvute ya muda kidogo, hatimaye Kamati ya
Mipango Miji na
Mazingira iliruhusiwa kufanya ziara ndani ya kiwanda cha Sadolini, na kujionea
mapungufu kadhaa; Wafanyakazi hawana vifaa vya kuzuia magonjwa kama maski na
buti, na pia mfumo mzima wa maji taka haukua katika mazingira rafiki
Mwenyekiti
wa Kamati ya Mipango Miji na Mazingira Mh. Sultan Salim,
akiteta jambo na Mfanyakazi wa Mastermind Tobacco Ltd,wakati akiiongoza kamati
kuingia kwenye sehemu ya uzalishaji wa kiwanda, wa kwanza kushoto ni Bw. Abdon
Mapunda, Mkuu wa Kitengo cha Mazingira(MEMO), akifuatiwa na Mh. Abdulkarim
Masamaki,Diwani Kata ya Kariakoo.