Na David Langa
Idara ya elimu msingi katika Manispaa ya Ilala chini ya
uongozi wa Afisa Elimu Mwl. Elizabeth Thomas Imeunda Vituo vya walimu
vilivyopewa jina la Klasta katika kanda nne ili kuweza kusogeza huduma karibu
na walimu katika maeneo yao ya kazi.
Vituo hivi vya walimu ( Klasta) vinaongozwa na maafisa elimu wasaidizi ambapo
kila kituo kitakuwa na kiongozi mmoja akishirikiana na waratibu wa Elimu kata
pamoja na walimu wakuu wa shule katika maeneo yao. Klasta zilizoundwa na wakuu
wake katika mabano ni Klasta ya Kimanga ( Bupe Kyungu), Klsata ya Gerezani
(Sarafina Mdami), Klasta ya Ukonga (Devota Stambuli ) na Klasta Chanika
inayoongozwa na Mwl.Nancy Peter
Klasta ya Kimanga inajumuisha kata za Kimanga,kata ya
Kinyerezi,Tabata, Segerea na kata ya Vingunguti, Klasta nyingine ni Klasta ya
Gerezani inayoundwa na Kata za Gerezani, Ilala, Upanga Magharibi, Upanga
Mashariki, Mchikichini, Kariakoo na Mchafukoge, kata zingine ni Kisutu,
Buguruni na kata ya Kivukoni. Klasta ya Ukonga inajumuisha kata za Ukonga,
Kitunda, Kivule,Kiwalani, Gongo la Mboto na Kata ya Kipawa. Klasta
ya nne ni Klasta ya Chanika ambayo inajumuisha kata nne za Chanika, Msongola,
Pugu na kata ya Majohe.
Kuundwa kwa vituo hivi vya walimu kwa kiasi kikubwa
kumepunguza adha ya walimu kusafiri umbali mrefu kuja katika ofisi za manispaa
kwani moja ya majukumu ya hawa maafisa Elimu wasaidizi ni kushugulikia baadhi
ya matatizo ya walimu ikiwa ni pamoja na walimu kuhakiki majina yao ya
kiutumishi na taarifa zingine kama za malipo ya likizo.
Akizungumza katika Kituo cha Ukonga inayoongozwa na Devota
Stambuli, Afisa Elimu Mama Thomas amesema lengo kuu ni kusogeza huduma karibu
na walimu katika maeneo yao badala ya walimu wote kufika katika ofisi yake ambapo
wakati mwingine wanapomkosa ofisini unakuwa ni usumbufu kwa walimu hao. Pia nasema ndani ya Manispaa ya
Ilala, idara ya elimu Msingi ndiyo yenye watumishi wengi kuliko idara zote
ambapo mpaka Machi 2014, idara yake likuwa na jumla ya waimu 3600 na hivyo kuwa
vigumu kuhudumiwa katika ofisi moja.
Jamani naomba muelewe ya kuwa ili kutekeleza malengo ya
matokeo makubwa sasa ni lazimu tuunde timu maalum ya kiutendaji badala ya
kuendelea kufanya kazi kwa mazoea tofauti na inavyoelekezwana na
serikali+alisema mama Thomas.
Pia liongeza kuwa katika Klasta hizi walimu hukutana na
kuonea kirafiki, kufahamiana na pia kubadilishana uzoefu kwani kazi ya ualimu
siku zote inahitaji kuongeza ujuzi na kujua mbinu mbali mbali wanazozitumia
walimu wenzako katika sehemu zao za kazi.
Chini ya mpango huu wa kugawa kanda za kiutendaji idara hii
ya msingi inahitaji kufanya tathmini ya mara kwa mara na kwa karibu na walimu ambao ndio wadau
wakubwa katika kuhakikisha taifa linapata jamii iliyoandaliwa kwa namna iliyo
sahihi.
Katika kutambulisha timu ya utendaji chini ya idara yake
afisa elimu huyo pia alimtambulisha Afisa utumishi anayeshugulika na walimu idara
ya elimu msingi Ndg. Robert Muna ili kurahisisha upatikanaji wa huduma na taarifa badala ya walimu wanaofika katika ofisi
ya mkurugenzi kutojua ni wapi pa kuanzia.
Bw. Muna kwa upande wake amewaahidi huduma safi na kwa
wakati ili kupunguza malalamiko ya walimu ili kuongeza hamasa na tija ya
kufanya kazi katika vituo vyao vya kazi.
Katika vituo hivi pia kumeundwa kamati mbali mbali
zitakazokuwa zinashugulikia mahitaji ya kiidara. Baadhi ya kamati hizo ni
Kamati ya taaluma, kamati ya mnazi mkinda, kamati ya tafrija na mikasa. Kamati
zingine ni kamati ya nidhamu na kamati ya uchumi ambapo kila kamati imepewa
majukumu ya kutekeleza na kisha kuziwasilisha kwa mkuu wa klasta ambaye
atazikusanya na kuzishugulikia kwa kadri ya mahitaji na maelekezo.
Akizungumzia baadhi ya changamoto zinazoikumba idara yake ni
madai ya muda mrefu ya walimu amabayo yanashugulikiwa na serikali kuu kwani
wapo baadhi ya walimu wamepandishwa madaraja lakini hawajalipwa stahili zao.
Hata hivyo Afisa Elimu Mama Thomas alitoa angalizo kwa walimu
wanaowasilisha taarifa zisizo sahihi hasa zile za likizo ambapo walimu wengi
wamekuwa wakiwasilisha taarifa zinazoonesha wanatoka mikoa ya mbali tofauti
walivyojaza kwenye taarifa zao za awali wakati wanapoajiriwa hali ambayo wakati
mwingine unachelewesha huduma pale inapotoka taarifa kinzani za mtumishi.