Na David Langa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Ndg. Mwendahasara Maganga
amefanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari 14 zitakazohusika kuchukua wanafunzi wa
kidato cha kwanza hasa wale wa chaguao la pili mwanzoni mwa mwezi wa nne mwaka
huu, 2014.
Ujenzi huo wa madarasa umetumia fedha za ambapo kiasi cha shilingi Bilioni Moja na
milioni mia saba(1,700,000,000) zimetengwa kwa ajili ya shughuli hiyo.
Katika ujenzi huo wa madarasa shule zilizohusika na idadi ya madarasa
katika mabano ni Furaha Sekondari (1),Zawadi sekondari (2),Ugombolwa (2),
Magoza (6), Ulongoni (8),Pugu Station (10)na Majani ya Chai sekondari madarasa
9.
Zingine ni Msimbazi Sekondari (8), Binti Musa (7)na maabara
1, Mchanganyiko (4),Juhudi Sekondari
(10), Ilala sekondari (6)na mchikichini madarasa manne ambapo katika
shule ya Sekondari Mwanagati imejengwa maabara kwa ajili ya masomo ya sayansi.
Mkugenzi aliwahimiza wakuu wa shule husika pamoja na kamati
za ujezi kuhakikisha ujenzi wa madarasa hayo unakamilika kwa wakati ili
itakapofika mwanzoni wa mwezi wa nne wanafunzi wapokelewe bila tatizo.
Pia Mkurugenzi aliwataka wakuu wa shule hizo kuwasiliana na
ofisi yake muda wowote pale ambapo kutatokea kikwazo toka kwa idara
zinazohusika na usimamizi wa ujenzi huo.
Katika ziara hiyo Mkurugenzi aliambatana na Afisa uhusiano wa Manispaa
ya Ilala Bi. Tabu Shaibu na Afisa Habari Ndg. David Langa.