HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA
TANGAZO
MKURUGENZI
WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA ANAWATANGAZIA KWA MARA NYINGINE TENA KUWA
NI MARUFUKU NA HAIRUHUSIWI KWA WAFANYABIASHARA NA WAKAZI WA ENEO HILI:-
1. KUTUNDIKA NA KUWEKA BIDHAA NJE YA MADUKA.
2. KURUDISHIA AU KUJENGA TENA SEHEMU
ZILIZOBOMOLEWA WAKATI WA OPARESHENI HII.
3. WAMACHINGA KUUZA AU KUTEMBEZA
BIASHARA MITAANI.
4. BABA AU MAMA LISHE KUFANYA BIASHARA
YA KUUZA VYAKULA MITAANI.
5. KUFANYA BIASHARA YA BODABODA NA
BAJAJ KATIKA ENEO LA CENTRAL BUSSINESS DISTRICT (CBD).
6. KUENDESHA MIKOKOTENI NA GUTA.
WALE WOTE WATAKAOKIUKA AMRI HII WATAKAMATWA NA KUCHUKULIWA
HATUA ZA KISHERIA IKIWA NI PAMOJA NA
KUFIKISHWA MAHAKAMANI.
OPARESHENI HII BADO INAENDELEA NA NI
YA KUDUMU
IMEANDALIWA NA KUTOLEWA NA MKURUGENZI
MANISPAA YA
ILALA