OPERESHENI
SAFISHA JIJI YASAIDIA KUPAMBANA NA MAJAMBAZI
- Milioni 3,420,000 zaokolewa
Na
Lucy Semindu –Kariakoo
Operesheni
safisha Jiji inayoendelea katika Jiji la Dar es Salaam imeleta mafanikio makubwa
kwani jiji sasa ni safi biashara holela zimepungua kwa kikasi kikubwa na barabara
zinapitika kisarahisi zaidi kuliko iliyokuwa awali.
Jambo
la kufarisha zaidi ni kuwa ulinzi na usalama umeimarika .Hayo yamejidhirihisha
pale Jeshi la Mgambo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi jana wapipofanikiwa
kuokoa shilingi milioni 3,420,000 ambazo
ziliporwa na majambazi katika duka la maua liliopo mtaa wa Aggrey na Sikukuu linalomilikiwa
na Bi Bodaa Chiang.
Aidha
kundi la majambazi walipora mfuko mdogo aina ya kisalfet aliokuwa ameshika BI Bodaa
Chiang baada ya kufunga duka lake hilo la maua mnamo Saa 11.30 alasiri jana.
Alipiga kelele ndipo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mgambo waliwakimbiza
majambazi hao na kufanikiwa kuokoa mfuko huo uliokuwa na fedha.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo bw. Kassim
Abeid alisema risasi zilisikika ambazo zilirushwa hewani katika tukio hilo na alipongeza Serikali kwa
hatua hii ya kusafisha jiji na kuondoa wafanyabiasahara wanaofanya biashara
katika maeneo yasiyoruhusiwa ambapo sasa imekuwa rahisi kupambana na uhalifu
kwa kuwa barabara na mitaa inapitika kirahisi
.
Naye
Bi Bodaa Chiang alishukuru Jeshi la Polisi kwa kupambana na majambazi na kuokoa
fedha zake ambazo zote zimepatikana bila kupotea. Zoezi la kuondoa wafanyabiashara
wanaofanya biashara katika maeneo yasiyoruhusiwa linaendelea.
Mfanyabiashara mwenye asili ya China akihesabu fedha zilizookolewa na maaskari kutoka Jeshi la Polisi na Mgambo katika kituo cha polisi msimbazi jana. ( picha na Lucy Semindu)
Mfanyanyabiashara akiangalia fedha zikihesabiwa