WAFANYABIASAHARA WAKAIDI ILANI ILIYOTOLEWA NA HALMASHAURI
YA MANISPAA YA ILALA
·
WAJENGA
UPYA VIBANDA VILIVYOBOLEWA
Na
Lucy Semindu – Vingunguti
Wafanyabiashara
wa Vingunguti wakaidi amri halali ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, iliyowataka
wabomoe vibanda vya biashara vilivyojengwa katika maneo yasiyorusiwa. Hayo
yameonekana wazi baada ya Manispaa ya Ilala kubomoa vibanda hivyo tarehe 14
aprili 2014 na wafanyabiashara hao kuvijenga upya tena.
Hali
imeifanya Manispaa ya Ilala kwenda leo kwa mara nyingine kuvibomoa vibanda
hivyo. Katibu Tarafa wa Ilala bibi Christina Kalekezi amesema ameshangazwa na
kitendo kilichofanywa na wafanyabisahara hao kwani wamekaidi amri iliyotolewa
na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
Kikosi
cha Jeshi la Polisi na la Mgambo kilionekana leo katika maeneo ya Vingunguti relini,
Machinjio ya Vingunguti na katika Reli iliyopo Buguruni kwa myamani wakivunja
vibanda vya wafanyabiashara vilivyojengwa katika maeneo yasiyoruhusiwa.
Hata
hivyo ilionyesha wazi kuwa walikwisha tangaziwa
kuviondoa vibanda hivyo, kwani sehemu nyingi bidhaa zilikuwa zimekwishaondolewa katika
vibanda. Mfanyabiashara wa relini njia ya kwa mnyamani ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, aliwashangaza
wengi pale kijiko cha Manispaa kilipotaka kuvunja kibanda chake.
Mfanyabiashara
huyo alianza kutweta na kusaidiwa na ndugu na jamaa zake kuondoa rundo la nguo zilizokuwa
zimejaa kwenye kibanda chake. Hata hivyo shughuli zilisimama kwa takriban
dakika kumi na tano ili aweze kuondoa nguo zote zilizokuwemo katika kibanda
hicho cha biashara .
Naye
Ndugu Joseph Manento amesifu sana zoezi hilo kwani sasa jiji ni safi na karibu
sehemu nyingi zinapitika kirahisi. Ameomba jitihada hizi za kurudisha hadhi
jiji la Dar es Salaam liendelee.
Kwa
upande wake Katibu Tarafa wa Kariakoo Bw. M. Muyenjwa amesema kuwa zoezi hili linaendelea na ni la
kudumu kwani jiji la Dar s Salaam linatakiwa liwe ni sehemu salama na safi. Imekuwa
ni desturi kwa wafanyabiashara kukaidi matangazo yanayotolewa ipo haja
wakazingatia maelekezo wanayopewa.
Greda likiwa katika harakati la kuvunja vibanda
wananchi wakiambiwa kutawanyika ili kuruhusu kazi inedelee vizuri
( Picha zote na: Lucy Semindu )