ADRA YATOA VIFAA VYA MAABARA, VITABU NA VIATU KWA SHULE ZA MANISPAA YA ILALA

 
 
Na Hashim Jumbe
Taasisi isiyo ya kiserikali ya ADRA imetowa vifaa vya maabara na vitabu vya kiada na ziada kwa shule za sekondari za Manispaa ya Ilala, pamoja na viatu kwa Wanafunzi wa shule za Msingi za Manispaa ya Ilala.
 
 
Mstahiki Meya  wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akisoma hotuba wakati wa ugawaji wa vifaa vya maabara na viatu kwa Wanafunzi wa shule za Manispaa ya Ilala.

Wanafunzi wa shule ya Msingi  Umoja wakicheza ngoma maarufu ya Makhirikhiri wakati wa shughuli ya ugawaji wa vifaa vya maabara na viatu.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Raymond Mushi mwenye suti nyeusi akijiandaa kupokea vifaa vya Maabara kutoka kwa Mkurugenzi wa ADRA.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Raymond Mushi akimvalisha Mwanafunzi viatu kuashiria kupokea viatu hivyo toka kwa ADRA

Wanafunzi wa shule ya sekondari Zanaki wakiwa na nyuso za furaha baada ya kupokea vifaa vya maabara kutoka ADRA, nyuma yao ni viongozi wa ADRA na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Raymond Mushi aliyepo katikati.

Baadhi ya Wanafunzi wa shule za msingi waliowawakilisha wenzao kupokea viatu walivyopewa na ADRA wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa ADRA na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Raymond Mushi na watatu kulia waliosimama ni M/Kiti wa Huduma za Jamii Manispaa ya Ilala Bi. Angelina Malembeka.

Picha ya pamoja ya viongozi wa ADRA na Mkuu Wilaya ya Ilala Mh. Raymond Mushi

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi