Na David Langa
Baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa pamoja limepitisha azimio la kubomolewa na kujengwa upya soko la Kisutu litakalokuwa na Gorofa 4 yenye sehemu ya soko na ofisi mbali mbali.
Ujenzi huo unatarajiwa kuanza rasmi mwezi April mwaka huu 2015,baada ya wadau wanaohusika kufikia muafaka wa wa garama za ujenzi ambapo kiasi cha shilingi Bilioni 11 zitatumika. Fedha hizo zinatolewa na Banki ya rasilimali nchini TIB kama mkopo wa masharti nafuu.
Baada ya kukamilika kwa soko hilo jumla ya wafanyabiashara 400 watanufaika tofauti na sasa ambapo wafanyabiashara waliopo ni 200.
Diwani wa kata ya Jangwani Mh. Abuu Jumaa akichangia mada katika baraza hilo. |
Kmanda wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (PCCB) kanda ya Ilala akitoa mada katika baraza hilo la madiwani ya namna ya kupambana na rushwa. |