Na David Langa.
Kamati mbili za usumbufu na Vibali vya vileo zinazoundwa na madiwani na watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala zimefanya ziara katika maeneo mbali mbali ndani ya Manispaa kuangalia kero za wananchi kuanzia kati kati ya jiji na maeneo ya pembezoni mwa mji.
moja ya mambo yaliyotiliwa mkazo na kamati hizo ni suala la wafanya biashara wadogo wadogo maarufu kama wamachinga ambapo kamati ya usumbufu ilipita maeneo ya kati ili kujionea hali halisi pamoja na suala utupaji na uzoaji taka.
kwa upande wa kamati ya vibali vya vileo iliyo chini ya Mstahiki meya, kamati hiyo ilifanya ukaguzi katika kata za Tabata, Segerea na Kinyerezi kukagua vibali vya uuzaji wa vinywaji vikali (pombe) pamoja na kuona kama wamiliki wa biasahara hizo wanafuata sheria kama zilivyoainishwa katika leseni zao ambapo kwa kiwango kikubwa wafanyabiashara hao kutozingatia sheria.
Baada ya kuona hali hiyo Kaimu mwenyekiti wa kamati hiyo Mh. Eva Nyamoyo aliagiza watu hao watozwe faini hapo hapo na wengine wanaoonekana kuwa sugu kufungiwa biashara zao shughuli hiyo iliendelea mpaka saa nne usiku kabla ya kuahirishwa ili kupangwa upya.
Wafanyabiashara wengi wa vileo wameonekana kufungua biashara zao kabla ya saa 12 jioni kwa siku za jumatatu hadi ijumaa, na saa kumi kwa siku za sikukuu, jumamosi na jumapili ambapo ni kinyume na sheria iliyoainishwa kwenye vibali vyao.
Mkuu wa idara ya mazingira na usafishaji Bw. Charles Wambura akitoa maelezo kwa mmoja wa Mh. Diwani ambaye ni mjumbe wa kamati ya usumbufu walipotembelea kata ya jangwani. |
kamati ya usumbufu ya manispaa ya Ilala wakikagua uchafuzi wa mazingira katika eneo la viwanja vya jangwani jijini Dar es salaam |

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mnispaa ya Ilala Bw.Isaya Mngurumi akikagua mkataba wa uzoaji taka kati ya Halmashauri na kampuni ya Green wastePro |
kamati ya vibali vya vileo ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ikifanya ukaguzi katika moja ya baa iliopo eneo la Kinyerezi kata ya Kinyerezi |
watendaji wakiendelea na ukaguzi wa vibali naq leseni kata ya Kinyerezi |

Meneja wa baa ya Kwetu pazuri akijitetea mbele ya kamati kabla ya kutozwa faini ya shilingi laki mbili kwa makosa mawili yaliyopatikana katika baa yake |