MATUKIO MBALI MBALI KATIKA PICHA

Mkuu wa kitengo cha mazingira wa Manispaa ya Ilala Ndg Abdon Mapunda akifanya ukaguzi katika kiwanda cha kuzalisha bidhaa mbali mbali za mafuta eneo Moshi bar kata ya Kivule. kiwanda hicho kimefungwa kutokana na kuchafua mazingira na pia kujengwa katika makazi ya watu kinyume na sharia ya mazingira.

Ndg Abdon Mapunda akiandika zuio kwa ajili ya kusimamisha uzalishaji katika kiwanda hicho kinachomilikiwa na raia wa China ambao hata hivyo hawakupatikana katika eneo la kliwanda. kushoto ni Afisa mazingira ndg Churchil Mujuni


Afisa Elimu idara ya elimu msingi Bi. Elizabeth Thomas akipeana mkono na mwenyekiti wa taasisi isiyo ya kiserikali ya OCODE katika hafla ya makabidhiano ya madawati 217 yenye thamani ya zaidi ya mil. 30 iliyotolewa na taasisi hiyo kwa shule za Tungini, Nzasa II na Viwege.
Mkababidhiano hayo yalifanyika katika shule ya msingi Tungini siku ya Ijumaa ya tarehe 23 Jan,2015. Kushoto ni mchumi wa manispaa ya Ilala Ndg.Rogasian Seda,aliyemwakilishi w mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala



Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Tungini kata ya Chanika wakifurahia baada ya kukabidhiwa madawati



wanafunzi wakiwa kwenye madawati yaliyotolewa na taasisis ya OCODE

Mwakilishi wa mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Rogasian Seda akitoa neon la shukrani kwa taasisi ya OCODE mara baada ya kupokea madawati 217.


Afisa Elimu msingi wa Mnispaa ya Ilala Bi. Elizabeth Thomas akiongea na waandishi wa habari baada ya kupokea madawati katika shule ya msingi tungini kata ya Chanika.

Afisa Elimu msingi akiongea na mwakislishi wa taasisi ya OCODE katika shule ya msingi Viwege baada ya kupokea madarasa matawi  yaliyojengwa na taasisi ya OCODE.

Muonekanao wa madarasa hayo yaliyojengwa na taasisi ya OCODE katika shule msingi Viwege kata ya Majohe, manispaa ya Ilala.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Ndg.Isaya Mngurumi akikagua vifaa vya usafi vya kampuni mbali mbali mbali yaliyopewa tenda ya kuzoa taka katika Manispaa ya Ilala

Baadhi ya vifaa vya usafi vinavyotumiwa na kampuni ya TIRIMA.



Baadhi ya vifaa vya usafi vinavyotumiwa na kampuni ya GREEN WASTE PRO.


Baadhi ya vifaa vya usafi vinavyotumiwa na kampuni ya AJM

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala akiondoka na ujumbe wake katika viwanja vya mnazi mmoja.
PICHA ZOTE NA DAVID LANGA

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi